Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo huku wakipaza sauti baada Sheikh Ponda kushinda rufaa ya kupinga hukumu ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam. Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, Mei 9, 2013. (Picha na Francis Dande).
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (wa pili kushoto) akitoka katika chumba cha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza wakati  akitoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ingekua vizuri kama lingetumia wapenda haki waliokusanyika nje ya mahakama badala ya kutumia neno wafuasi, taswira kama hizi ni kawaida kupatikana hasa ktk mashitaka yenye utata kama ambavyo tumeona watu wakikusanyika ktk kesi ya Sapi Fundikira, Jide,Seya,Kesi za Mh.Mtikila juu ya Tanganyika,na nyingi zinginezo si wafuasi ni wapenda haki...huyu bwana hana wafuasi...

    ReplyDelete
  2. Lazima angeshinda tu! kuna kesi za kushinda na kushindwa hata kama zina au hazina hatia.


    Serikali lazima iogope kumhukumu tifauti sheikh huyu








    ReplyDelete
  3. How can you call that justice

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...