Sintofahamu iliyotokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma Ijumaa Novemba 28, 2014 imepelekea Spika Anne Makinda (pichani) kulazimika kusitisha shughuli za Bunge mpaka hapo watapojadiliana tena. 

Hii ni baada ya majadiliano makali kuhusu kuwajibishwa ama la kwa viongozi wanaohusika na sakata la akaunti ya Escrow. Hali hii iliibuka baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA na kambi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe kuinuka na kusema kuwa Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, na kwamba kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kutoka maamuzi kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. 
"Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi", alisema Mhe. Mbowe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi hata kwa akili nyepesi Chenge anaweza kushauri lolote kwa suala kama lile ambalo naye ni mhusika (kesi ya nyani akimu ngedere) Watanzania tunaongopewa kweupe.
    Ninaloweza kusema ni MUNGU ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...