Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete salamu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa furaha na ujumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Washington DC uliomtembelea kumjulia hali na kwasilisha salamu maalumu za pole  za Rais Barack Obama jijini Baltimore, Maryland.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na maafisa waandamizi  wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington D.C. wakati walipomtembelea mjini Baltimore Maryland ambapo balozi Liberata Mulamula aliwasilisha kwa Rais Kikwete Salamu maalum za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. Picha na Freddy Maro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana wa Jumatatu, Novemba 24, 2014 amepokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Marekani Mheshimiwa Barak Obama.

Katika salamu zake Rais Obama ameelezea kufurahishwa na taarifa kwamba Rais Kikwete anaendelea vyema kiafya baada ya kufanyiwa upasuaji kwa mafanikio na kuondoa tatizo la tezi dume alilokuwa nalo.

Rais Obama amesema katika salamu hizo kuwa alipata heshima kufanya ziara rasmi nchini Tanzania mwaka 2013, na pia kumualika Rais Kikwete kwenye mkutano wa  Marekani na viongozi wa Afrika mwaka huu.

“Nakutakia kasi ya kupona kabisa na nataraji kuendelea kufanya kazi nawe katika masuala tuliyokubaliana ya kipaumbele”, amesema Rais Obama kwenye salamu zake hizo. 
Rais Kikwete amekabidhiwa salamu hizo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula, aliyekuwa ameongozana na maafisa waandamizi wa ubalozi waliofika Baltimore kumjulia hali. 
Mhe. Mulamula amesema salamu kutoka sehemu mbalimbali duniani zimekuwa zikimiminika ubalozini kwa njia mbalimbali. 
Taratibu za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zilikamilika Jumatatu, Novemba 24, 2014 asubuhi baada ya  madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, kumfanyia  hatua ya mwisho ya tiba. 
Rais Kikwete ameendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani. 
Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014. 
Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014. 
Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

25 Novemba,2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa anaonekana ni mwenye nguvu,mchangamfu, na mwenye afya njema. Mwenyezi Mungu azidi kukutia nguvu.

    ReplyDelete
  2. Wishes you all the best, take care of your self

    ReplyDelete
  3. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuzidi kumjaalia afya njema, Mhe. Rais wetu mpendwa.

    Uholanzi

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa pole sana,mungu akupe nguvu,wananchi wako tunakusubiri urudi,angalau utusaidie kurekebisha maana hali ya hewa imechafuka sana sakata la ESCROW.

    ReplyDelete
  5. Kila la kheri mh. Rais
    Seoul
    Korea kusini

    ReplyDelete
  6. Mh jk pole kwa kuumwa, lakini hawa jamaa uliowachagua wakusaidie kazi wanakuangusha, njoo uwatimuwe kazi, wewe kila siku unatuangaikia wananchi wako ili tupate maendeleo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...