Kushoto ni Dkt. Frank Forka ambaye ni mkurugenzi PGCEDC Africa Trade Office akielezea njia za kufuata kwa mwekezaji kutoka Tanzania anapokuja kutafuta au kufanya mazungumuzo na wawekezaji wa Kimarekani kwa ajili ya kuingia nao ubia kwa ajili ya kuwekeza Tanzania. Dkt. Frank Furka alisema jambo la kwanza muhimu ni kujifunza utamaduni wa wafanyabishara wa Kimarekani hasa inapokuja kwenye swala la muda, Mambo mengine ya kuzingatia ni ufafanuzi wa kina na uwazi wa fulsa unayoitafutia mwekezaji na itakapokuja swali uwe na uwezo wa kulijibu kwa ufasaha.
Caroline Chang kutoka Maryland Center For Foreign Investment akielezea sheria ya EB-5 Invester's Program inavyoweza kumnufaisha mwekezaji kutoka Tanzania anayewekeza nchini Marekani.
Kulia kwa Jessca Mushala ni Mujuni Joseph Kataraia akielezea kampuni ya Urban and Rural Engineering Services Ltd na aina gani ya mwekezaji wanaemtafuta kuingia nae ubia wa uwekezaji wa umeme wa jua na vifaa vya ujenzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Acha kuandika kwa makosa mahali kama hapa, nimekerwa neno FURSA kuandikwa FULSA. Huu ni ujinga wa hali ya juu sana

    ReplyDelete
  2. Siku hizi hakuna anayejali kusahihisha makosa ya lugha. Kuna tofauti kati ya lugha: unavyoandika na unavyozungumza. Inasikitisha kuona hata serikali haifanyi jitihada yoyote ya kuimarisha kiswahili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...