Afisa Masoko wa Silafrica bwana
Alpesh Patel akikabidhi ufunguo wa gari aina ya Suzuki Carry jijini Dar
leo kwa Mama Fatuma Wahenga kutoka kampuni ya FMJ Hardware,ambaye
aliibuka mshindi wa pili kupitia promosheni iliyojulikana kwa jina la
Uza na Ushinde.
Afisa Masoko wa Silafrica bwana Alpesh Patel akizungumza kwa ufupi kuhusiana na promosheni yao iliyojulikana kwa jina la Uza na Ushinde na namna washindi wanavyopatikana.
======== ======= =======
Kampuni ya Silafrica Tanzania Ltd, inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya
plastiki leo imemkabidhi gari aina ya SUZUKI CARRY mshindi wa pili wa shindano
la Uza na Ushinde ambaye ni Mama Fatuma
Wahenga kutoka F M J Hardware.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi
zawadi hiyo Jijini Dar es Salaam Afisa Masoko wa Silafrica bwana Alpesh Patel alisema promosheni iliwahusu mawakala wote wa
bidhaa za SIMTANK kwa lengo la kuhamasisha ubunifu na kujituma miongo mwa
mawakala hao.
“tunawashukuru mawakala wetu kwa
juhudi zao na kujitoa katika kuuza bidhaa zetu, hivyo promosheni hii ililenga
kuheshimu mchango wao, natumia fursa hii kuwashukuru mawakala wetu wote walioshiriki
katika promosheni hii kwa kujitoa kwao na kufanya kazi kwa juhudi” Alisema
Patel.
Bwana Alpesh pia alimshukuru Mama Wahenga kwa juhudi
zake katika mauzo na kuwaomba mawakala wengine kuongeza bidii ili kujiweka
katika nafsi ya zawadi kutoka SIMTANK siku zijazo.
Akipokea zawadi hiyo Mama Wahenga
alishukuru SIMTANK kwa zawadi na juhudi zao katika kuboresha maisha ya
mamilioni ya watanzania wanotumia huduma za maji safi na salama yaliyohifadhiwa
katika tanki imara na salama SIMTANK kutoka Silafrica.
“Kwanza nawashukuru, nitatumia gari hili
kupandisha mauzo yangu kwa kuwafikia wateja wengi kwa wakati hivyo nitatimiza ndoto zangu za kuwa wakala kiongozi
katika biashara ya kuuza SIMTANK.” Alisema, Mama Wahenga.
SIMTANK walianza biashara yao miaka 20 iliyopita kwa
lengo la kutoa huduma za kuhifadhi maji safi na salama katika vyombo imara
salama na vyenye ubora katika nchi za Tanzania na Kenya, Kwa sasa SIMTANK ndiyo
bidhaa inayoongoza na kuaminiwa katika soko kwa matumizi ya tekinolojia ya hali
ya juu na matumizi ya malighafi imara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...