Dk Cuthbert Maendaenda akiwatwanga lekcha wahariri mbalimbali mjini Morogoro |
ULAJI wa supu ya pweza, karanga mbichi, muhogo mbichi, mbata kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume kumeelezwa kuwa ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita kwa kuwa haina uhusiano kati ya urijali wa mwanaume na virutubisho vinavyotolewa na vyakula hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Dk Cuthbert Maendaenda wakati akitoa mada yake katika semina ya wahariri iliyofanyika mkoani Morogoro iliyojadili nafasi ya wanaume katika kuleta mabadiliko katika jamii juu ya afya ya uzazi na ujinsia.
Dk Maendaenda ambaye alikuwa akijibu maswali pia kuhusiana na dhana hiyo iliyozoeleka kuhusu nguvu ya supu ya pweza, alisema ipo haja ya wanaume kuangalia sababu za kudorora kwa uwezo wao na kufanya marekebisho badala ya kudhani kwamba kuna dawa kutoka katika vyakula hivyo.
Miji mingi nchini kwa sasa nyakati za jioni kuna supu ya pweza na mauzo ya karanga mbichi ambao wauzaji wamekuwa wakinadi kama msaada wa kurejesha heshima katika ndoa.
Alisema ufanyaji mapenzi unaathirika na vitu vingi na jamii lazima kuangalia ukweli huo ili kuwa na watu wanaojiamini katika mapenzi na wale ambao wanamatatizio kupata ushaudi wa kidaktari.
Mwezeshaji huyo kutoka Taasisi ya sweden inayohusu haki za afya ya uzazi na ujinsia (RFSU) tawi la Tanzania ambalo linaendesha mradi wa TMEP wenye lengo la kuwaamsha wanaume kuwa chachu ya mabadiliko na hivyo kuwa na uelewa mpana kuhusu haki za ujinsia.
Watanzania sijui kwanini tuna mawazo finyu hivyo. Kila wakati ni kuwaza na kufikiria URIJARI tu, kuna mambo mengi ya kufanya kwenye maisha kuliko kuupa kipaumbele URIJARI. Tuwe na vision, angalieni holistic zaidi kuliko afya ya kitu ambacho siyo issue. Ningependa kuona watu wanafikiria wanaweza kujizuiaje kupata kisukari, moyo, Hepatitis, kuzuia mimba za utotoni, kuzuia vifo vya wanawake wenye mimba na vifo vya watoto kabla ya miaka mitano n.k. Kufikiria udume-udume siyo priority.
ReplyDeleteUsijali mdau tutaanza kuongelea ushoga kama nchi zilizo brainwashed you lol
ReplyDeleteMuongo huyo hata hajui anachokisema, asome professional forum za watafiti vitu vyote vilivyotajwa hapo vina uhusiano wa moja kwa moja.
ReplyDeleteSex ni sehemu ya maisha yetu, whether you like or not just because tuna mambo mengine ya kufanya sijui kwanza yapi hayo anayoyasema mchangiaji hapo juu tusifikirie sex. Mwanaume kama sio rijali hata hizo pesa unamtafutia nani!!!
Kote duniani watu wanatafuta pesa ku spendi na famila zao, beutiful women hakuna zaidi ya hapo megine utatudanganya tu...!
Kwa nini wewe Annony hapo juu unawahukumu watanzania wote kwa hisia zako tu? Jisemee wewe mwenyewe sio kuwahusisha watu wote kwenye hayo uyasemayo!
ReplyDelete