Dkt Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji akiongea kwenye
kongamano la uwekezaji kwa mikoa ya ukanda wa ziwa Tanganyika
lililofanyika mjini sumbawanga mwishoni mwa wiki. hawapo pichani
washiriki wa kongamano hilo
Washiriki wa kongamano la uwekezaji ambao ni wawekezaji kutoka ndani
na nje ya nchi wakifuatilia kwa umakini mjadala wa kongamano hilo
kwenye uwanja wa Nelsoni Mandela Mjini Sumbanga Mkoani Rukwa.
Na Kibada Kibada Rukwa.
Waziri wa Uwekezaji na uwezeshaji Dkt Mary Nagu amezishauri Taasisi
za Kifedha hasa mabenki kupunguza riba inayotonzwa wakati wa kuomba
mikopo ili kuwezesha wawekezaji Mwekezaji wa ndani na nje kukopa na
kupata mitaji itakayomsaidia kuweza kuwekeza.
Alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati wa Kongamano la Uwekezaji
kwa Mikoa ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika unaojumuisha mikoa ya Rukwa,
Katavi na Kigoma lililofanyika kwenye viwanja vya Nelsoni Mandela
Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Kongamano hilo lilihudhuriwa Viongozi mbalimbali, Mabalozi
wanaowakilisha nchi zao hapa nchiniWawekezaji kutoka ndani na nje ya
nchi, pamoja na wananchi wa mikoa ya ukanda wa ziwa Tanganyika hasa
wakazi wa mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa na lilifunguliwa na Makamu wa
Rais Dkt Ghalib Bilal.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...