Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika Tarehe 30 Novemba, 2014 Nairobi, Kenya. 

Kwa mujibu wa Mkakaba Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri la
Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Tarehe 20 – 27 Novemba, 2014 katika  ngazi ya Wataalam, Makatibu Wakuu na Mawaziri. Aidha, katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa uwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha mwaka mmoja na Jamhuri ya Kenya inayomaliza kipindi chake, Ikiwa ni utekelezaji wa Ibara ya 12 (2) ya Mkataba wa Uanzishaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akizungumzia Tanzania kuchukua Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo alisema, “Katika kipindi cha uenyekiti wake, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendeleza mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi cha uenyekiti wa Jamhuri ya Kenya. Aidha, mkazo utawekwa katika kuhakikisha mtangamano wa Afrika Mashariki unaendelezwa kwa kuzingatia matakwa ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya pamoja na Kanuni na Taratibu za Jumuiya. 

Aidha, mkazo utawekwa katika kuhakikisha Sekta binafsi na Wadau wengine wanashirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa mtangamani wa Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuzitumia fursa zitokanazo na Jumuiya ya Afrika Mashariki,”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...