Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania , Profesa, Sospeter Muhongo (kushoto) na Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi, Mhe. Come Manirakiza wakitia saini mkataba wa miaka 50 wa usafirishaji wa umeme kutoka Mradi wa Rusumo kwenda nchini humo katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Mradi huo unazihusisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo (kushoto), akibadilishana hati na Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi, Mhe Come Manirakiza, baada ya kutiliana saini mkataba wa miaka 50 wa usafirishaji wa umeme kutoka Mradi wa Rusumo kwenda nchini humo katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Mradi huo unazihusisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.
Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe Issa Mtambuka (wa pili kushoto mbele) akiwa na maofisa wengine kwenye sherehe hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...