Tanzania leo imekabidhiwa rasmi Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki baada ya Kenya kumaliza muda wake wa kipindi cha mwaka mmoja. 
Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta na Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo walipokea Uenyekiti huo katika Mkutano wa Baraza wa Mawaziri uliofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC), Jijini Nairobi, Kenya. 
 Rais wa Tanzania anatarajiwa kupokea Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki siku ya Jumapili katika Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya utakaofanyika pia hapa KICC.
Waziri Samuel Sitta akizungumza baada ya kupokea Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki leo 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo akisoma taarifa ya Kamati ya Makatibu Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Baraza la Mawaziri. Wengine kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera, Waziri Mh. Samuel Sitta na Mwandishi wa Taarifa za Mikutano Mpya kutoka Uganda Bi. Mary Nankabirwa.
Mwenyekiti anayemaliza muda wake Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Kenya Bi. Phyllis Kandie (katikati) kabla ya kukabidhi uenyekiti kwa Waziri Samuel Sitta wa Tanzania. Kushoto ni Bw. Mugisha Kyamani kutoka Tanzania ambaye alikua ni Mwandishi wa Taarifa za Mikutano kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita

Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akliwa na  Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora Mh. George Mkuchika (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (kulia).
Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughilikia Miundombinu Dkt. Enos Bukuku walipokutana Jijini Nairobi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki leo. Wengine ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora Mh. George Mkuchika (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (kulia).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...