Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng. Ngosi Mwihava
akizungumza kabla ya kuanza kwa mnada wa kwanza wa madini yaliyokamatwa
yakisafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.Wengine katika picha ni
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania (TMAA), Bruno Mteta (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri wa Madini Tanzania, Richard Kasesera (wa pili kulia), Kamishna
Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim (wa
tatu kushoto), Meneja Usafirishaji Madini wa TMAA, George Kaseza (wa
pili kushoto), na maafisa wengine kutoka TMAA, Eng. Charles Shamika
(wa nne kushoto) na Flora Kisena (wa kwanza kushoto).
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania (TMAA), Bruno Mteta (wa nne kulia), akisoma moja ya zabuni
(bid) ya ununuzi wa madini yaliyokuwa yakipigwa mnada jijini Arusha.
Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini,
Eng. Ngosi Mwihava (wa tano kulia), Zabibu Napacho, Afisa Mfawidhi Ofisi
ya TMAA-Arusha (wa kwanza kulia), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari
TMAA, Eng.Yisambi Shiwa (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri
wa Madini Tanzania, Richard Kasesera (wa tatu kulia), Kamishna Msaidizi
wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim (wa tatu
kushoto), Meneja Usafirishaji Madini wa TMAA, George Kaseza (wa pili
kushoto), na Eng. Charles Shamika (wa nne kushoto), Flora Kisena (wa
kwanza kushoto) kutoka TMAA.
wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria Maonesho ya
Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha, wakishuhudia mnada wa kwanza wa
madini yaliyokamatwa yakisafirishwa nje ya nchi bila kuwa na vibali
husika.Aliyenyanyua karatasi ya maombi ya zabuni (bid) ya madini hayo ni
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania (TMAA), Bruno Mteta.
Meneja Usafirishaji Madini kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania
(TMAA), George Kaseza (katikati),akizungumza na waandishi wa habari
mkoani Arusha, mara baada ya kumalizika kwa mnada wa kwanza wa
madini yaliyokamatwa yakisafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.
Na Teresia Mhagama
Madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100 yaliyokamatwa wakati
yakisafirishwa nje ya nchi bila kufuata taratibu za nchi za usafirishaji madini
yamepigwa mnada na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).
Madini hayo yamepigwa mnada jijini Arusha katika Maonesho ya Tatu ya
Kimataifa ya Vito yaliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru ambapo mnada
huo wa kwanza kufanyika nchini ulishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini, Eng.Ngosi Mwihava, Mwenyekii wa Bodi ya
Ushauri wa Madini, Richard Kasesera, Makamishna Wasaidizi wa Madini
nchini na wananchi waliohudhuria maonesho hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...