Habari wadau, naomba kuwajulisha kuwa mazishi ya aliyekuwa mwanachama mwenzetu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani, aliyefariki jana, yatafanyika kesho alasiri katika makaburi ya Sinza, Dar es Salaam.
Tunaomba tushirikiane katika kuhifadhi mwili wa mpendwa wetu, ambapo sekreterieti ya TASWA imemteua Majuto Omary ambaye ni Mwenyekiti wa TASWA FC, Mwani Nyangassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Zena Chande Mhazini Msaidizi kusimamia michango mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari za michezo nchini kwa ajili ya msiba huo.
Nawasilisha,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
20/11/2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...