Shirika lisilokuwa la kiserikali
linalojihusisha na uhifadhi wa mazingira na wanyama pori la World Wide Fund for
Nature (WWF), limejiunga katika jitihada za kitaifa na kimaifa za kupambana na
ujangili nchini ambapo pamoja na mambo mengine limetoa mabango yanayotahadharisha
wananchi na wageni waingiao na watokao Tanzania kutojihusisha na shughuli
yoyote inayohusiana na ujangili wa wanyama.
Akikabidhi vifaa hivyo Novemba 27,
2014 jijini Dar es Salaam kwa Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki,Mkurugenzi wa
WWF Tanzania Bw. Bell'Aube Houinato,aliwataka jumii ya za ndani na za kimataifa
kuhakikisha zinaongeza jitihada ili kuhifadhi rasilimali hizo kwa manufaa ya
sasa na kizazi kijacho.
" Jukumu la kumaliza kadhia hii
ya biashara haramu ya nyara za umma ni la wote si la serikali pekee au WWF bali
umma mzima wa Tanzania na kimataifa,hivyo kila mmoja kwa sehemu yake na eneo
lake awajibike ipasavyo",alisema Bw.Houinato.
Aidha,aliongeza kuwa ni jukumu la
kila mmoja wetu kuhakikisha vyombo vinavyohusika na ulinzi na uangalizi wa
rasilimali zetu vinajengewa uwezo wa kimaarifa na kivifaa ili kuhakikisha
vyombo vyote vinatimiza wajibu wake kwa tija kubwa.
Kwa miaka ya hivi karibuni nchini
Tanzania,kumeibuka tatizo la ujangili ambapo mauaji a Tembo na Faru
yameongezeka huku jitihada za kimataifa na kitaifa zikiwa zinaonekana
kulegelega jambo lililozishtua jamii za kimataifa hivyo kujiunga na kuongeza
bidii katika vita hiyo.
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki
(kulia), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa hafla
ya kukabidhiwa mabango yanayotahadharisha wananchi na wageni waingiao na
watokao Tanzania kutojihusisha na shughuli yoyote inayohusiana na ujangili wa
wanyama (kushoto), Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw. Bell'Aube Houinato.PICHA NA PHILEMON SOLOMON
Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw.
Bell'Aube Houinato akisisitiza jambo kuhusiana na vyombo vinavyohusika na
ulinzi na uangalizi wa rasilimali za nchi.
Waandishi wa habari
wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki (meza kuu kulia), wakati wa
hafla hiyo.
Mkurugenzi wa WWF Tanzania Bw.
Bell'Aube Houinato (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam ,Bw.Moses Malaki moja
ya mabango hayo.
Muonekano wa moja ya mabango hayo
yenye luga tatu ambayo yatawekwa sehemu mbalimbali ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere wa jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...