Tarehe 9 Desemba 2014, ripoti ya mwaka ya dunia ya malaria (World Malaria Report 2014) ilizinduliwa rasmi katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za bunge la Uingereza zilizopo Portcullis House, Westminster jijini London.
Katika hafla hiyo, Tanzania ilitajwa kama mfano wa nchi inayoendelea kupata mafanikio barani Afrika katika kupambana na ugonjwa wa Malaria hasa kwa upande wa Zanzibar.
Tanzania ilipongezwa kwa mchango wa kisiasa wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika kuhakikisha agenda ya mapambano dhidi ya Malaria inapewa kipaumbele na katika eneo la utafiti wa kisayansi unaofanyika katika Taasisi ya Utafiti ya Ifakara.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa mtoto wa Malkia, Prince Andrew. Wengine waliohudhuria ni pamoja na wabunge kutoka vyama vya kisiasa nchini Uingereza,wawakilishi wa taasisi za kitafiti na wadau kutoka sekta binafsi. Tanzania iliwakilishwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe.
Balozi wa Tanzania, Mhe. Peter Kallaghe, akichangia machache katika hafla fupi ya Uzinduzi wa Ripoti kuhusu Malaria Duniani, uzinduzi huo ambao ulifanyika katika Ofisi za Bunge la Uingereza.
Balozi wa Tanzania, Mhe. Peter Kallaghe, akimsikiliza kwa makini mmoja wa wawakilishi wa Ripoti kuhusu Malaria Duniani, katika uzinduzi ambao ulifanyika jana katika Ofisi za Bunge nchini Uingereza.
Balozi wa Tanzania, Mhe. Peter Kallaghe (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawakilishi kutoka shirika la Afya Duniani na washiriki wengine katika Uzinduzi wa Ripoti kuhusu Malaria Duniani, uzinduzi ambao ulifanyika tarehe jana tarehe 9 Desemba 2014 katika Ofisi za Bunge la Uingereza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...