Picha na habari na  Owen Mwandumbya, Dodoma 
 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeandaa Bunge la Vijana linalofanyika Mjini Dodoma kwa siku tatu, ikiwa ni jitihada la kuwajengea uwezo vijana wa vyuo vikuu nchini. Bunge hilo liloanza vikao vyake juzi linalojumuisha Vijana kutoka Vyuo Vikuu 15 vya hapa Nchini vinavyozunguka mkoa wa Dodoma. 
 Bunge hilo linalotarajiwa kumalizika tarehe 3 Desemba, 2014, ni sehemu ya Mpango wa Elimu kwa Umma ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kupitia mradi wake wa kuwezesha uwezo wa wabunge na watumishi unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), umelenga kuwajenga vijana kushiriki masuala ya kibunge kwa vitendo. 
 Jumla wa wanafunzi 120 kutoka vyuo vya UDOM CBE, MIPANGO, TIA, MZUMBE St. John, VETA, Theophili kisanji - Mbeya, MKAWA, RUAHA, chuo cha kiislam Morogoro, Tumaini, na Chuo cha Sayansi Mbeya wamechaguliwa kuwa wabunge wa Bunge hilo.
 Spika wa Bunge la Vijana Ndg. Edgar Israel kutoka chuo cha St. John cha Dodoma akiingia Bungeni tayari kwa kuanza kwa Bunge hilo
 Mpambe wa Bunge akiweka siwa mezani tayari kwa kuanza vikao vya Bunge la Vijana
 Spika wa Bunge la Vijana Ndg. Edgar Israel kutoka chuo cha St. John cha Dodoma akisoma dua kabla ya kuanza kwa Bunge hilo mjini Dodoma. Waliosimama mbele yake ni Makatibu Mezani.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...