Wapenzi wa burudani  ya muziki wa kizazi kipya na muziki wa taarabu watapata burudani ya funga mwaka kutoka kwa gwiji wa muziki wa kizazi kipya ambaye anatamba kwa vipao mbalimbali vipya Diamond Platnumz na mfalme wa muziki wa taarabu Mzee Yusuf  na kundi lake la Jahazi Modern Taarab watapanda jukwaa moja katika”Tamasha Wafalme”litakalofanyika katika ukumbi wa Dar Live,Mbagala jijini Dar es Salaam.
Tamasha hili  la wafalme ambalo limeanza kuwa gumzo la  jiji kutokana na kuwa na burudani za aina mbalimbali kwa ajili ya kukonga nyoyo za wapenzi wa burudani  limedhaminiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu amesema kuwa Vodacom imeamua kudhamini tamasha hili  kwa ajili ya kuwapatia furaha na burudani wateja wake na  wananchi kwa ujumla katika msimu huu wa sikukuu ya Krismas na mwaka mpya.
“Kama ilivyo kauli mbiu yetu kuwa“ukiwa na Vodacom maisha ni murua”tunahakikisha mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wetu pia tunajua kuwa kuna muda wanahitaji kufurahi kwa burudani  hivyo ndio maana tunadhamini matamasha ya  aina hii na tutaendelea kufanya hivyo siku zote ikiwa ni moja ya njia ya kusema ahsante kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono”Alisema. 
 Mbali na tamasha la wafalme, Nkurlu alisema kampuni hiyo imeandaa matamasha makubwa ya burudani ya wazi yatakayofanyika katika ufukwe wa bahari Coco Beach moja litafanyika Desemba 26 na lingine litafanyika siku ya mwaka mpya ambapo wanamuziki wanaotamba nchini watashiriki  kutoa burudani.
Naye mratibu wa tamasha la wafalme Abdala Mrisho amesema kuwa wapenzi wa muziki wategemee kupata burudani ya funga mwaka ambayo itaacha historia katika mwaka huu kwani imeandaliwa katika hadhi ya kimataifa.Alisema katika kuhakikisha wananchi wanapata burudani ya kutosha tamasha litaanza saa tano asubuhi mpaka saa tisa usiku na kiingilio kitakuwa shilingi elfu kumi na kwa wale watakaopenda tiketi za VIP ni 20,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...