Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika mashindano ya Kitaifa ya Riadha ya wilaya ambayo yanatarajiwa kufanyika katika kiwanja cha Amaani Disemba 26-27 mwaka huu.

Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Rais Shein kwa lengo la kukuza sekta ya michezo nchini yametayarishwa na Baraza la michezo la Taifa Zanzibar (BMTZ) kwa kushirikiana na chama cha Riadha (ZAAA) Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa baraza la michezo Bi Sharifa Khamis katika ukumbi wa wizara ya habari , utamaduni, utalii na michezo huko kikwajuni wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema mashindano hayo yatakayozishirikisha Wilaya zote 10 za Unguja na Pemba yatajumuisha wanariadha 250 ambapo michezo yote ya riadha ikiwemo kukimbia masafa ya mita 100 , 200, 400, na 1500 kwa wanawake na wanaume itafanyika. Aidha ameongeza kuwa jumla ya vikundi 12 kutoka Kenya , Uganda na Tanzania Bara vimealikwa kushiriki Mashindano hayo.

Amefahamisha kuwa sambamba na Riadha pia kutakuwa na michezo ya kurusha mkuki , tufe, ,na kisahani. Amebainisha kuwa Washiriki wa mashindano hayo watapatiwa huduma zote za michezo bure ikiwemo malazi , mavazi ya michezo , chakula, usafiri na zawadi zote za washindi za vikombe , medali na fedha taslim.

“Lengo kuu la mashindano hayo ni kuinua mchezo wa riadha Zanzibar kuanzia vijijini , maskulini na maeneo mengine mbali mbali kwa nia ya kutafuta vipaji vya wanariadha kutoka katika sehemu hizo ili kuviendeleza vipaji hivyo “ alisema Bi Sharifa.

Amesema dhamira ya Rais wa Zanzibar ni kuona Zanzibar inarejesha hadhi yake ya asili ya ubingwa katika michezo tofauti ambayo amesema sifa hiyo imepotea kwa kipindi kirefu ikilinganishwa katika miaka 70.

Mashindano hayo nisehemu ya utekelezaji wa sera tya michezo Zanzibar , ambayo inasisitiza kuwa vyama vyote vya michezo Zanzibar vifanye jitihada za makusudi za kuinua michezo ili nchi iweze kupiga hatua kubwa katika michezo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Bi Sharifa Khamis akizungumza na Wanahabari kuhusu Mashindano ya kitaifa ya Riadha yatakayofanyika Disemba 26-27 mwaka huu katika Ukumbi wa wizara ya habari Kikwajuni mjini Zanzibar. Rais Shein anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi wa Mashindano hayo. Picha na Makame Mshenga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...