Na Asteria Muhozya, Nzega 
Mgodi wa Resolute uliopo Wilayani Nzega Mkoani Tabora jana tarehe 12 Desemba, 2014, ulikabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma katika hafla fupi iliyofanyika na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia madini Stephen Masele.
Wengine walioshuhudia ni, Mkuu wa Wilaya ya Nzega aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Bituni Msangi, Viongozi Waandamizi wa Wilaya ya Nzega, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Kamati ya Kitaifa ya uchimbaji, Uongozi wa Juu wa kampuni ya Resolute na wananchi.  Naibu Waziri Masele alieleza kuwa, tukio la kukabidhiwa eneo hilo la Mgodi kwa Chuo ni tukio ambalo limefungua ukurasa mwingine kutokana na kwamba Chuo cha Madini Dodoma kitaiwezesha Tanzania kuzalisha wataalamu zaidi waliobobea katika tasnia hiyo ambao mchango wao kwa taifa unahitajika katika kuendeleza sekta ya madini.
 “Tunataka wanafunzi wasome kwa vitendo, hii itawezesha kupata wataalamu waliobobea. Ni nafasi kwa wanafunzi na Chuo cha Madini kuitumia fursa hii vizuri. Najua kuna mawazo mchanganyiko ya kupoteza mapato kwa Halmashauri na mengine ya kupata Chuo lakini, kufunga mgodi ni sehemu ya Sheria ya madini”, aliongeza Masele.
 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi, akizungumza katika halfa hiyo, alieleza kuwa, Mgodi wa Resolute una historia ya kuwa mgodi wa kwanza nchini kuzalisha madini ya dhahabu na kuogeza kuwa, ndani ya kipindi cha miaka 12 cha uhai wa mgodi huo umeweza kuchangia kiasi cha shilingi bilioni 290 za Kitanzania ikiwa ni kodi mbalimbali zilizotolewa na mgodi huo kama mrahaba. 
Aliongeza kuwa, Halmashauri iliweza kupata kiasi cha shilingi bilioni 6 ikiwa ni kodi na kiasi cha Tsh bilioni 6 kilitumiwa na mgodi huo kuwezesha za kijamii ikiwemo ujenzi wa zahanati, shule, upatikanaji wa huduma safi ya maji katika eneo linalozunguka mgodi huo. 
Pamoja na eneo la mgodi huo kukabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma, vilevile mgodi umekabidhi majengo, mitambo, maabara ambapo, kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo cha Madinini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile alieleza kuwa, eneo hilo litatumiwa na wanafunzi wa mwaka wa pili kwa ajili ya masomo ya vitendo. 
Mgodi wa Resolute umefunga rasmi shughuli zake za uchimbaji madini ya dhahabu katika eneo hilo, ambapo ulianza kazi zake mwaka 1998. Kabla ya makabidhiano hayo, mgodi huo umefanya ukarabati, ujenzi wa madarasa, na uhifadhi wa mazingira.
 Sehemu  mgodi ambao shughuli za uchimbaji zilikuwa zikifanywa na mgodi wa Resolute ambao pia umekabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma. Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe ameeleza kuwa,mgodi huo utatoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu shughuli za uchumbaji.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Mhe Stephen Masele (aliyesimama katikati na pama) akishuhudia halfa fupi ya kusaini makabidhiano ya eneo la Mgodi wa Resolute kwa Chuo cha Madini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile, katikati ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Resolute Peter Beilby. Wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi (wa pili kuchoto aliyesimama),Mkurugenzi Kampuni ya Resolute Rose Aziz na baadhi ya waliohudhuria.
 Meneja Mazingira   baada Mgodi wa Resolute Jackie Sinclair (Kulia), akimkabidhi funguo mbalimbali za majengo ya eneo la mgodi wa Resolute Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini)  Stephen Masele (Kushoto) mara  makabidhiano ya eneo la mgodi.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe funguo mbalimbali za majengo ya mgodi wa Resolute kwa ajili ya Chuo cha Madini Dodoma. Picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Isiwe ajabau tumeachiwa mashimo tu! A capitalist is to make money: more money. No social responsibility for environmental pollution!

    ReplyDelete
  2. Wameacha na pesa ya kufukia hayo mashimo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...