Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa 2014 Idris Sultan akishangilia wakati akilakiwa kwa furaha na mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo akitokea nchini Afrika Kusini yalikokuwa yakifanyika mashindano hayo. Kushoto kwake ni Laveda aliekuwa mshiriki mweza wa Idris.
Idris akionekana ni mwenye furaha kubwa sana baada ya kuwasili nchini.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi (kati) akijadiliana jambo na Mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idris Sultan pamoja na aliekuwa mshiriki wa shindano hilo, Laveda, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...