Na Sultani Kipingo
Inasemekana kila jina lina asili yake na maana pia. Hata hilo jina lako ulipewa kwa sababu, na lina asili yake. Kama si la kutoka katika Biblia ama Quran, basi ni la kimila lenye kumaanisha jambo, kama vile siku, tukio, mahali ama hata shida au raha aliyopata mama wakati wa uzazi wako.
Jiji la Dar es salaam  zamani liliitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyelipa jiji hili jina "Dar es Salaam" linalotokana na lugha ya Kiarabu  (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili yanayofanana katika Kiarabu yaani "dar" (=nyumba) na "bandar" (=bandari).
Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo pana ya mto Kurasini. Kuanzia 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala. Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu 1904 ziliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara kuwa koloni ya Tanganyika chini ya Uingereza.
Bado kuna mabishano ya ni nini hasa asili ya jina Africa. Wengine wanadai linatokana na neno la Kigiriki la APHRIKE, lililomaanisha kusikokuwa na baridi, ama la Kilatini APRICA, lenye kumaanisha nchi yenye jua daima.

 Wengine wanasema neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Waroma wa Kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo katika jimbo la Carthage ama Tunisia ya leo tu. Asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile.
Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini ya Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).
Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara. Jina la "Afrika" limekuwa kawaida kuanzia karne ya 16 BK.
Misri ya wakati huo ilikuwa inachukuliwa kama sehemu ya bara la Asia,na alikuwa Mwanajiografia aitwaye Ptolemy (85-165A AD) ambaye aliigawa Afrika na Asia na Ulaya kwa kuchora ramani inayoonesha Suez na Bahari Nyekundu kuwa ndio mpaka baina ya Asia na Afrika.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ahsante kwa fundisho. I knew about how Dar-es-Salaam got it's name, but 'Afrika' was new to me. Thank you very much for this lesson. Like I always say...'you learn something new everyday'! Proud to be an African.

    ReplyDelete
  2. Mkuu Sulatani kipingo, napingana nawe kwa kusema kuwa neno la Afrika lilitokana na neno la kilatini sio kweli kabisa. Ukweli neno hili la Afrika limetokana na lugha za Absinia siku Ethopia,katika jamii za lugha Amharic,neno Farikya walilitumia kama sehemu iliyobarikiwa au mahala pa kwenda kujitakasa nafsi,walatini na wazungu wengine walishindwa kutamka Farikya wa taanguliza "A" na kundoa a mbele F,wakaita AFRIKA. na kama kawaida ya watu wa ulaya ufupisha maneno kwa kutaka ubwete mfano hujambo wanasema Jambo

    ReplyDelete
  3. tunakushukuru kwa taarifa hii. lakini nadhani jina la ehiopia ni karibu ni sana. enzi za kale jina hilo halikuwepo bali lilikuwepo jina la sabaa au sheba ikijumuisha nchi za ethiopia, eritrea, djibouti na yemen. na eneo hilo lilifanya sabaa empire au pia huitwa sheba empire.

    baadae jina la sabaa au sheba likabadilika na kuitwa habash au kwa kiswahili uhabeshi. ehiopia ilijulikana kwa jina la habash kwa karne nyingi wakati huo. habash pia ilikusanya eritrea, djibouti na ethiopia za leo bila ya yemen.

    jina la ethiopia kama lijulikanavyo sasda ni jipya limeaza karne chache zilizopita na haliepo wakati wa tawala za wayunani wa kale au warumi.

    hatahivyo shukran kwa kumbu kumbu uliyotuletea.


    ReplyDelete
  4. Eh watu munajua historia ya mambo!

    Tupeni elimu na sisi tufaidike.

    ReplyDelete
  5. jamaa anawasema wenzie wanafupisha neno "hujambo" kuwa "jambo", bora hao kuliko wewe unaepotosha maneno kwa kuandika "ufupisha maneno" badala ya "hufupisha maneno"........ kaa kando kuliko kupotosha kiswahili

    ReplyDelete
  6. fix tu, mnajua asili ya Misri na Mji wake mkuu kuitwa Cairo? Basi zamani watu walikuwa wanapunga hewa ufweni mwa bahari mara akatokea "kaa" aka lobster watu wakaanza "Kaa iloo" "Kaa iloo" na kumkamata yule lobster. Wengine wakaanza "mi sili" hata "mi sili". Ndio nchi ikaitwa "Misri" na mji mkuu "Cairo"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...