Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa tahadhari kwa wananchi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa wakati wa zoezi la marudio ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 21/12/2014 katika baadhi ya vituo vya kupigia kura jijini Dar es Salaam.

Awali, uchaguzi huo ulifanyika nchini kote tarehe 14/12/2014 na kulazimika kuahirishwa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura kutokana na sababu mbalimbali. Katika mkoa wa Dar es Salaam uchaguzi huo uliahirishwa katika vituo mbalimbali kama ifuatavyo:

Aidha, Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulivu kama ulivyopangwa. Kutakuwa na askari waliovaa sare nadhifu, na askari wa kiraia ambao watakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa wakati wote amani inatawala katika vituo vya kupigia kura. Askari hawa watatumia weledi wa hali ya juu ili zoezi hilo liendeshwe kwa utulivu mkubwa ikizingatiwa vituo ni vichache ikilinganishwa na uchaguzi wa tarehe 14/12/2014.

ONYO:
Wananchi wanatakiwa kutofanya yafuatayo katika siku ya kupiga kura:
1. Kutofanya kampeni yoyote siku ya kupiga kura.
2. Kutovaa mavazi yanayoonyesha ushabiki kwa chama chochote cha siasa.
3. Kutovunja sheria yoyote, kanuni, na taratibu zinazotawala uchaguzi wa serikali za mitaa
4. Kufuata sheria za nchi ikiwemo sheria mama yaani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977

Aidha, yetote atakayekwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu zilizopo atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa mahakamani.
“UTII WA SHERIA BILA SHURUTI NI MUHIMU KUZINGATIWA WAKATI WOTE”

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...