Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani Kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Bw. Japhet Kembo akifurahia huku akipongezwa na wanachama na wapenzi wa Chadema mara baada ya kuibuka mshindi wa Kiti cha Mwenyekiti kwa Kupata Kura 510 huku CCM wakiwa wamepata kura 215 na NCCR kupata kura 205

 Mawakala wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Migombani wakihesabu kura ambapo sanduku hilo ndio lilikuwa sanduku la mwisho kuhesabiwa katika Kituo cha Kupigia kura cha Migombani ambao wakazi wa Mtaa wa Migombani walikuwa wakisubiria matokeo

Baadhi ya wapita njia nao ilibidi wasimame maana uchaguzi huu ulivuta hisia za watu wengi kutokana na hali iliyoonyeshwa na wakazi wa mtaa huo kukaa mpaka dakika za mwisho

 Msimamizi wa Uchaguzi katika Kituo cha Kupigia Kura cha Migombani akitangaza Mshindi wa Uchaguzi huo uliomalizika kwa Mgombea wa Chadema akiwa ameibuka Mshindi kwa Kupata Kura 510 huku wapinzani wake wakiwa na Kura 215 za CCM na Kura 205 za NCCR

 Wakazi wakishangilia kwa Ushindi. 
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...