Wananchi wakiwa wamemzunguka Kakakuona aliyeonekana asubuhi majira ya saa moja maeneo ya Kigamboni Kisiwani Mtaa wa Chaboko ambapo kwa mujibu wa ripota na mpiga picha wetu Salma Bob Kassim, mnyama huyo aliwekewa Unga, ndizi, maji pamoja na pesa.
Lakini akaishia kunywa maji tu kabla ya kukimbilia vichakani. Wananchi kwa mamia waliofurika kumuona Kakakuona huyo walisikika wakisema kuwa huenda huo ni utabiri kwamba huenda mvua zikawa nyingi msimu huu.
Polisi walifika eneo la tukio na baada ya kuona hakuna uvunjifu wa amani wakatoa taarifa kwa maafisa wa Maliasili ambao walifika na kumtia mnyama huyo kwenye kiroba na kuondoka naye

Kakakuona akijikunja baada ya umati wa watu kuzidi kuwa mkubwa
Baadaye, huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha, Kakakuona huyo alielekea vichakani huku umati ukiendelea kumshangaa. Baadaye watumishi wa Maliasiali walifika na kumtia kwenye kiroba na kuondoka naye.
Picha na Salma Bob Kassim
Picha na Salma Bob Kassim
Kuna ushahidi gani wa kisayansi wa kuunganisha kuonekana kwa kakakuona na kuwepo na mvua,baraka nk.au ndio jamii imekwama katika karne ya analog?
ReplyDeleteLahaula ivi bado tupo ktk zama hizi....walau basi angetokea mmoja mwenye kukumbuka kadhia ya maisha kisha kuweka bendera au nembo ya ukawa na ccm.
ReplyDeleteWatu wanataka maji acheni kukariri kila siku kakakuona nawekewe maji,unga na fedha.....mungeweka nembo ya ukawa na ccm, vingine vyote vingejileta vyenyewe baada ya jinamizi kuwatoka....mkumbuke hivyo basi ndio nishawakumbusha huku nilipo kakakuona wapo ila sio dili.....
ReplyDelete