Na Anitha Jonas – Maelezo, Kagera
Kikundi cha vijana cha Ngara Youth Foundation chenye wanachama wapatao kumi na moja waliomaliza elimu ya juu wamenufaika baada ya kupata mkopo wa Milioni tano kupitia mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kuanzisha miradi miwili ikiwemo mradi wa kuuza mbao na mradi wa kuosha magari.
Hayo yalisemwa jana na Katibu wa kikundi hicho Bw. Jason Athanas alipotembelewa na maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutathimini miradi inayoendeshwa na vikundi baada ya kupatiwa mkopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kutokana na changamoto ya ajira iliyopo nchini.
Kikundi hicho kimeishukuru Serikali kwa kuwapatia mkopo uliopelekea kuongeza kipato kwa kila mwanachama hivyo kuboresha hali ya maisha baada ya kukosa ajira na kuwafanya kuwa wabunifu katika jamii.
“Tuliamua kuanzisha kikundi hiki baada ya kumaliza chuo na kutafuta ajira kwa muda mrefu hivyo tuliamuamu kuungana kuanzisha kikundi chetu ambapo tulibuni mradi tulioona unafaa na kuomba mkopo, kwa sasa tuna miradi miwili ambayo ni mradi wa kuuza mbao na wakuosha magari (Car Wash)”,alisema Bw. Athanas.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Habari, Vjana, Utamaduni na Michezo Bibi.Verdiana Mushi, aliwapongeza vijana hao kwa juhudi kubwa wanazozifanya na kutoa wito kwa vijana wengine kuiga mfano wa vijana hao kwa kuanzisha vikundi vyao na kuomba mkopo katika mfuko wa maendeleo ya vijana unaosimamiwa na Wizara.
Aidha Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Eliakim Mtawa aliwashauri vijana wa Ngara Youth Foundation kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu huku wakizingati matumizi mazuri ya mapato yanayotokana na miradi yao pamoja na kuendelea kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha kukua kiuchumi na kukuza miradi ya kikundi.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Ufutiliaji na Tathimini kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi.Verdiana Mushi akikagua
mradi wa kikundi cha vijana kutoka Ngara alipowatembelea kwa ajili ya
kutathmini maendeleo ya mfuko wa maendeleo wa vijana. Kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha Hekima Group
Ngara Bw.George Kessy
Katibu
wa Ngara Saccoss Bw.Joackim Jordan (wapili
kushoto) akiwaonyesha Maafisa kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo walipowatembelea hivi karibuni baadhi ya tofali
aina ya "vibrated blocks" zinazotengenezwa
kwa udongo na simenti ambazo vikundi kumi vya vijana vilipata mafunzo ya
kutengeneza matofali hayo kama sehemu ya
miradi wanayofanya. Kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha Hekima
Group Ngara Bw.George Kessy.
Picha
na Anitha Jonas - Maelezo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...