Na Sultani Kipingo 
Goli la kusawazisha lililofungwa kwa kichwa na Martin Skrtel (pichani) dakika saba ndani ya muda wa nyongeza leo umewapa Liverpool ushindi waliostahili dhidi ya Arsenal katika uwanja wao wa nyumbani wa Anfield. 

Refa Michael Oliver aliongeza dakika tisa kufuatia mpira kusimama kwa muda mrefu baada ya Skrtel kuumizwa na kupatiwa huduma ya kwanza baada ya kugongana kwa bahati mbaya na Olivier Giroud wa Arsenal. 

Giroud alionekana tayari kaipaisha Arsenal kuelekea kwenye kulipiza kisasi cha kupigwa bao 5-1 hapo hapo Anfield msimu uliopita baada ya kufunga bao la kuongoza, baada ya Mathieu Debuchy kusawazisha sekunde chache kufuatia bao la Liverpool la kuongoza lililofungwa na Philippe Coutinho dakika moja kabla ya mapumziko. 
Lakini Skrtel, akiwa amefungwa bandeji kubwa kichwani huku Liverpool wakiwa watu 10 kufuatia mchezaji wa akiba Fabio Borini kutolewa nje kwa mchezo mbaya, alipaa hewani na kuweka kimiani mpira wa kona uliopigwa na Adam Lallan dakika ya 97 na kumpita kipa Wojciech Szczesny mbele ya mashabiki maarufu wa Bwawa la Maini - The Kop.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Sultani Kipingo wewe si mkereketwa ila mfurukutwa wa Bwawa la mananihii!
    Duh kumbe ile 2-2 kwa Livapulu ulikuwa ushindi waliostahili? E bwana mshkaji Kipingo nakuvulia kofia.
    Lakini ndivyo reaction baada ya kipenga cha mwisho ilivyoonesha; wakati sisi Gunners tukiondoka vichwa chini kwa kukosa pwenti tatu, wenzetu Livapulu walishangilia ile mbaya yake utadhani wametwaa ubingwa!
    That tells you the whole story!
    Hongereni Bwawa la Maini kwa ushindi MNONO leo jioni!
    Mndengereko Ukerewe

    ReplyDelete
  2. YOU WILL NEVER WALK ALONE!!!

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juu wa Arsenal usiwe na wasi wasi mtachukua kikombe cha nafasi ya nne maana kila mwaka huwa mnakishangilia kuliko washindi wa kwanza

    ReplyDelete
  4. Tuna kikombe tayari. Ni timu pekee ambayo haibabaiki babaiki na vikombe wala usajili.
    Yet ina mvuto wa kipekee.
    Yet tunapozungumza mshabiki wa kila timu hujisikia kujibizana nasi, wivu umewajaa.
    Yet kila timu hutaka kununua wachezaji wetu.
    Si watu wengi wanaoelewa maana ya kucheza Champions League na wewe mdau hapo juu ni mmoja wao.
    Ukiacha timu zilizopigwa mnada Uingereza, ni Gunners pekee day in day out iko Champions League.
    Mshamba we!
    Mdau Ukerewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...