Na John Gagarini, Chalinze 
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete Ijumaa alifanyiwa sherehe za kijadi za kabila la Kikwere kijijini kwao Msoga, kwa mujibu wa mila za hapo.
Sherehe hizo,  ambazo ziliendana na kukabidhiwa vitu mbalimbali vya kijadi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, ni jadi ya Wakwere ambapo mtu baada ya kupata uongozi hutambikiwa na kukaribishwa rasmi kwenye kundi la wazee wa kijiji. 
Baadhi ya vitu alivyoakabidhiwa na mzee wa kabila hilo Zaidi Rufunga ni pamoja na kitanda cha kamba, msuli, kigoda na kinu pamoja na vitu mbalimbali. Sherehe hizo za kijadi ziliamabatana na ngoma ya Kikwere na ulaji wa chakula kiitwacho Bambiko ambacho hutumiwa na kabila hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete kushoto akipata maelekezo kabla ya kuanza kula chakula cha kabila la Kikwere kiitwacho Bambiko wakati wa sherehe za kijadi za  kumkaribisha katika kundi la wazee kwenye kijiji cha Msoga zilizofanyika juzi.
Mzee Zaidi Rufunga kulia akimkabidhi vyungu mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete wakati wa sherehe za jadi za kumkaribisha nyumbani zilizofanyika juzi kijiji cha Msoga. 
Kulia mzee Zaidi Rufunga akimuelekeza jambo kabla ya kula chakula cha jadi cha kabila la Wakwere kiitwacho Bambiko wakati wa sherehe za jadi za kumkaribisha nyumbani Ridhiwani Kikwete zilizofanyika juzi kijijini hapo.
Baadhi ya akina mama waliohudhuria sherehe za jadi za kumkaribisha mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani KIkwete zilizofanyika Ijumaa kijijini Msoga.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kushoto na katikati diwani wa kata ya Msoga Mohamed Mzimba na baadhi ya wageni wakila chakula cha jadi kiitwacho Bambiko mara baada ya sherehe za jadi za kumkaribisha nyumbani kwenye Kijiji cha Msoga 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. huo ugali na kuku ndio unaitwa bambiko?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...