Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis
Mkotya ametunukiwa Shahada ya Sayansi ya Jamii katika
Siasa, Uongozi na Utawala (Political Scince and Public
Administration), baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu
ya juu.
Mkotya pamoja na wahitimu wengine walitunukiwa shahada
zao mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya 26 ya Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika eneo la Bungo,
Kibaha mkoani Pwani.
Wahitimu wote walitunukiwa shahada zao na Mkuu wa
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk. Asha Rose Migiro,
ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria.
Katika mahafali hayo, mgeni rasmi alikuwa Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd. Wengine ni
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette
na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho Profesa Samuel
Wangwe.
Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya (kati) akiwa na wahitumu wenzake wakipia kitabu cha ratiba ya mahafali yao hayo.
Pongezi kutoka kwa ndugu waliofika kwenye mahafali hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...