Na Bakari Issa,Dar es Salaam

ALIYEKUWA Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG),Ludovick Utouh amesema mihimili mitatu iwekewe mipaka na kuangalia isiingiliane katika utendaji wake wa kazi kuruhusu kwake kuingiliana ni kufanya serikali isitawalike.

Hayo amesema leo jijini Dar es Salaam katika kupokea tuzo ya uadilifu kutoka kwa Kampuni ya Dream  Success Enterprises kutokana na kutambua umuhimu wa utendaji wake wa kazi.

Alisema kuwa mihimili mitatu isipojua mipaka yake itawaweka wananchi washindwe kujua uwepo wa mihimili hiyo na kufanya nchi ishindwe kutawalika kutokaka na mihimili hiyo kuwa na mianya ya kutoafikiana katika utendaji..

Utouh alisema kuna vitu hataweza kusahau katika ofisi ya CAG moja ni fedha zilizochotwa katika akaunti za nje (EPA) pamoja na ripoti ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, David Jairo ambapo wabunge walishindwa kujua uhalali wa fedha zilizochangishwa  na Jairo na hakuna sheria yeyote iliyovunjwa.

“Tuzo hii nimepata lakini nimepita  katika kipindi ambacho jina la ufasadi limeweza kuzaliwa kutokana  na uchotaji wa fedha za EPA na kufanikisha zingine kuweza kurudi, nchi zingine huwa zinashindwa kabisa kurudisha fedha za namna hiyo”alisema Utouh.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Andika habari zilizokamilika. Hiyo mihimili mitatu ni ipi???

    ReplyDelete
  2. Kama hujui mihimili mitatu nenda shule: Serikali, Bunge na Mahakama!

    ReplyDelete
  3. Wewe ndio uende shule ujifunze jinsi ya kuandika article zilizokamilika. Kumbuka sababu ya kuandika ni kutoa habari na kuelimisha jamii. Hujiandikii wewe binafsi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...