KIKOSI cha Usalama Barabarani  nchini  kwa kushirikiana na Chama cha Kutetea  Abiria Tanzania (CHAKUA) limesema wataendelea kudhibiti upandishaji wa holela wa nauli  za mikoani kuelekea katika sikukuu za kufunga mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Mohamed  Mpinga amesema watachukua hatua kali kwa mawakala wataopandisha nauli za mikoani.

Mpinga alisema kikosi cha usalama barabarani kimejipanga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora usafiri kwa bei zilizopangwa pamoja na kutoa onyo kwa madereva wanaoendesha mabasi na magari kufuata sheria za usalama barabarani.

“Hatutavumilia mawakala na madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani yote haya ni kutaka wananchi wetu wasinyanyasike katika kipindi cha sikukuu siku zijazo sheria zimewekwa na lazima watu wazifuate”alisema ,Mpinga.

Aidha alisema wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano pale watapoona wanaopandisha nauli ili kuweza sheria ichukue mkondo wake kukaa kimya kwa wananchi kunafanya jeshi kushindwa kuwabana watu wanaofanya hivyo.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed R. Mpinga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu abiria kutoa taarifa kwenye mamlaka husika ili watetewa na fedha  zao ziweze kurudishwa hata kama ni Tsh. 100/=.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...