Mshambuliaji Mpya wa timu ya Yanga, Danny Mrwanda amevunja ukimya kwa kusema hakutaka kusajiliwa Simba kwa mali kauli anachoangalia na 'njuru'.

Mrwanda ambaye ameanza mazoezi na Yanga jana jioni na kukabidhiwa jezi namba 24 alisema walishindwana dau na Simba  hivyo anaangalia kwenye maslahi.

"Mpira ni kazi yangu, naishi kwa ajili ya kutegemea mpira, sasa wao wameleta longo longo, Yanga wamekuja nikawapa dau wakakubali nikasaini mkataba, sasa hivi maisha yangu ni Yanga na akili zangu naelekeza kwenye timu yangu mpya na si mambo mengine, ninachangamoto ya kuhakikisha Yanga hawajuti kunisajili.

Kuhusu kusaini mkataba wa miezi sita Simba kama kocha wa wekundu hao wa Msimbazi Patrick Phiri alivyowahi kusema wiki iliyopita alisema "Nilifanya mazungumzo na Simba, na Phiri ananitaka hata leo hii, lakini viongozi wake longo longo, wanataka kunipa hela wanayotaka wao, hapo ndio tumeshindwana."alisisitiza Mrwanda huku akigoma katu katu kutaja kiasi alichoitaji Simba wakashindwa kumpatia.

Hata hivyo Mrwanda alisema kuwa mkataba wake wa  Polisi Morogoro ambayo inadai Yanga imemsajili mchezaji huyo kinyemela alisema "Habari za mkataba wangu na Polisi nisingependa kuzungumzia, viongozi wa Yanga watamalizana wenyewe na Polisi."alisema.

Naye kocha wa Yanga Mbrazil Marcio Maximo alisemaa ameshafanya kazi na Mrwanda wakati akiinoa timu ya Taifa, Taifa Stars, anamjua vizuri Danny na anajua ni kitu gani anaweza kukipata kutoka kwa mchezaji huyo.                                                                                                                                                                                                    
"Mrwanda ni mshambuliaji mzuri ana uwezo wa  kumiliki mpira, kukimbia katika nafasi, kufunga na kupiga pasi. Ingawa Danny ana udhaifu wake, hasa kuinama sana chini, ninalitambua tatizo hilo na nitalifanyia kazi, naamini ataifanya safu yangu ya ushambuliaji iwe yenye kasi zaidi.

Katika mazoezi ya jana jioni, Maximo aliweka wazi kikosi chake cha kwanza ambacho kitaanza katika mechi ya Nani mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao Simba ambapo langoni alisimama Deogratius Mushi 'Dida'  Juma Abdul, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub 'Canavaro' Mbuyu Twite, Simon Msuva, Emerson de Oliveira Neves Roque, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima na Andrey Coutinho.

Katika mazoezi hayo ambayo Maximo alitumia mfumo wa 3-4-3  huku wapiga penati katika kikosi hicho ni  Canavaro, Msuva, Ngassa, Joshua na Mrwanda, kwa maana hiyo, katika mechi hiyo ya Jumamosi Ngasa na Mrwanda wataingia wakitokea benchi na kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza na Andrey Countinho   .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hapa mnyama lazima akae atake asitake muda atakao kuwemo uwanjani Msuva,Ngassa,Mrwanda, Nyonzima kwa pamoja na hasa kama itakuwa dk 30 second half ongeza na Telela mnyama lazima afe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...