Kaka michuzi habari za jumapili. Pole na hongera kwa kazi nzuri unayofanya. kaka mimi ninaomba unisaidie kuweka hili jambo hadharani. Kuna mtu mwenye email adress yakimusi200@outlook.com. huyu mtu amekuwa akituma email kwa watu hasa walioko kwenye ndoa . anachofanya yeye anahack email za watu anaowataka na kuanza kuwatumia email kuwaambia kuwa wenza wao wanacheat. 
Nashindwa kuelewa yeye lengo lake linakuwaga ni nini. nikupe kisa kimoja. mimi na mdogo wangu na mkewe tuna kampuni yetu na tunafanya kazi pamoja.mwezi wa nane akamtumia mdogo wangu meseji kuwa mkewe anamcheat anatembea na boss wake huko anakofanya kazi while kazi tunafanya wote pamoja. 
But the way anavyomwongelea huyo wifi yangu ni kwamba inaonekana anamjua maana wifi yangu ni mjamzito akamwambia hiyo mimba itakuwa sio ya kwako maana kuna boss anatembea naye hapo anakofanya kazi. sasa tukashangaa kazi tunafanya wote information anazotoa mbona sio za kweli? mdogo wangu akaignore but akawa bado anaendelea kumtumie hizo emails.
Last week akamtumia mume wa rafiki yangu email akamwambia mkewe anamcheat  eti  so awe mwangalifu sana. akamwambia anampenda ndio maana ameamua kumtumia huo ujumbe.

Sasa kaka michuzi huyu mtu anakuwa ana lengo gani na watu na familia zao?au starehe yake inakuwa akiona ndoa imevunjika ? na hata ikivunjika yeye anafaidika nini? naamini huwa anawatumia watu wengi sana naomba uiweke hii hadharani ili watu wawe na tahadhari na huyu mtu  na kama hajaoa au kuolewa aingie kwenye ndoa apate experience ndio ajue cha kufanya ni nini sio anatumia watu email za kijinga namna hiyo.
Ni matumaini yangu kaka uatiweka hii haraka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nashauri mutume malalamiko yenu kwenye tume ya mawasiliano labda wataweza kumfuatilia na kuchukua hatua.

    ReplyDelete
  2. Duh hii kali na ni HATARI sana km isingekuwa wanafanya pamoja nyumbani nadhani pangekuwa padogo
    Watu wa namna hii naona wanaongezeka wengine wanatumia simu kutuma jumbe kama vile muna mambo yanayoendelea.
    poleni wote yalowafika hayo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...