Na Fredy Mgunda,Iringa

MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa,  Frank Kibiki,  ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Iringa mjini, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa Habari leo  ofisini kwake, Kibiki amesema ni wakati wa vijana kushika hatamu kwa kuwania nafasi mbali mbali, ndani ya CCM na hatimaye kwenye umma wa watanzania.

Kibiki ambaye ni Katibu mwandamizi wa Umoja wa Vijana, katika wilaya mbali mbali nchini amesema ameamua kuomba kupitishwa nafasi hiyo na CCM ili aweze kusaidiana na wananchi wa manipaa ya Iringa katika kuwaletea maendeleo.

Mjumbe huyo wa Mkutano mkuu wa ccm Taifa, amedai kuwa zipo changamoto nyingi zinazowakabili vijana na wananchi kwa ujumla na kwamba, njia pekee ya kuzitatua ni kuwa na uwakilishi toka miongoni mwao kwenye vyombo vya maamuzi.

Kitaaluma, Kibiki ni mwandishi wa habari mwandamizi kupitia magazeti ya Uhuru na Mzalendo, mkoani Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...