BAADA ya mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga kwa mchezo wa soka, Wafalme wa muziki wa dansi nchini bendi pizani za Msondo Ngoma na  Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae) nao watakuwa na Mtani jembe yao   siku ya Krismasi katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.

Mpambano huo wa Mtani Jembe umeandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu ya Krismasi na kufunga mwaka 2014.
Mpambano na bendi hizo, utasindikizwa na wakongwe wenzao wa muziki wa dansi nchini Vijana Jazz Band, wakiwa na binti wa aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo Hemed Maneti, Komweta Maneti ambaye ataimba nyimbo zote zilizokuwa zikiimbwa na baba yake.
Kapinga alisema kuwa pia pambano hilo litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wawili wa muziki wa dansi nchini kwa mwaka huu wa 2014.
Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kuondoa malalamiko ya kuhujumiwa.
“Tutakuwa na michezo aina mbalimbali ya watoto,” alisema Kapinga.
Alisema mchuano huo utaanza saa nane mchana hadi liamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...