Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, amesema habari zinazodai kuwa Serikali inataka kuwaondoa wakazi wa zaidi ya 40,000 katika eneo la Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha hazina ukweli wowote.
Novemba mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza, liliandika habari kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai wanaoishi eneo hilo.
Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.
Akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai wilayani Ngorongoro mwishoni mwa wiki, Nyalandu alisema habari hizo hazina ukweli wowote isipokuwa zina lengo la kuchafua taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa.
Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao.
“Nami niwahakikishie wanajamii wa Loliondo, Ngorongoro na wanajamii wote wa kimasai ambao wametishiwa nyau, kuwa serikali ya Tanzania haina mpango wowote wa kumfuata na kumfukuza mtu yoyote,” alisema.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akijaribu kurusha mkuki alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akitoka nje ya nyumba ya kimasai alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Mh Waziri akanushe na issue ya kutumia kibali cha Raisi kuwindia wanyama wetu
ReplyDelete