Bango la Ujenzi wa Barabara ya Lupaso-Bujesi ambayo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara ya Katumba -Tukuyu kwa kiwango cha lami.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais - Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya (katikati) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo,Said Mderu wakipata maelezo ya ujenzi wa barabara ya Lupaso-Bujesi ambayo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara ya Katumba -Tukuyu kwa kiwango cha lami.Wakati walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais - Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo,Said Mderu wakikagua ujenzi wa barabara ya Lupaso-Bujesi ambayo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara ya Katumba -Tukuyu kwa kiwango cha lami.
Ujenzi wa barabara unaendelea.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais - Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya (wa tano kulia), na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo,Said Mderu (wa tatu kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakadarasi na wahandisi wa ujenzi wa barabara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mkuu Mwandosya nilitaka kukushangaa kuona miaka yote hii umekaa serikalini lakini Mwakaleli-Katumba na vile vile Lwangwa Tukuyu hamna lami. Na huu ndiyo msingi mkubwa ambao unanivutia kugombea Ubunge 2015, ili(siyo nijaribu) bali niwatimizie watu wa Rungwe, angalau, njia ya lami. Wasafiri wa Mwakaleli na Lwangwa wanapata shida sana mvua zinyeshapo. Jamaa wa Arusha wametupita Mbeya kimaendeleo utadhani atuko taifa moja,ambapo namba ya wasomi karibu tupo sawa. Nakupa ongera kwa ilo Mmbunge. Ili jambo limechelewa sana, lakini afadhali linatimia. Nawaambia wapiga kura wote wa Rungwe sasa ni wakati wakumchagua mtu kwa jinsi anavyoleta maendeleo, siyo maneno pekee bali vitendo vya kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...