Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik na kulia ni katibu wa Baraza la wazee wa Dar es Salaam Mzee Mtulia.
Baadhi ya wazee na wananchi wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akilihutubia taifa kupitia wazee wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Picha na Freddy Maro. 
Picha zaidi BOFYA HAPA
Kupata Hotuba yote BOFYA HAPA

Bofya Link hiyo kumsikiliza 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Ankal Michu,
    Dondoo ziko wapi? You are left far away behind na blog zingine sasa! Unataka msaada?

    ReplyDelete
  2. Video please..thanks.

    ReplyDelete
  3. Ni nini raisi ameongea kwenye huo mkutano na wazee wa Dar?

    ReplyDelete
  4. It is a shame, maprofesa na Drs wanahujumu nchi. Hivi hawana hata huruma, sisi hatuna madawa, madawati etc, wao wanagawana tu hela za umma utafikiri peremende. Jamani hivi tunaelekea wapi? Sioni future ya gesi au mafuta, mapato yataliwa na wajanja kama hawa. Good on you JK, wafukuze wote.

    ReplyDelete
  5. How bad can it get, from UN Habitat to possibly Ukonga or Keko.

    ReplyDelete
  6. Sababu za mama T kufanywa kondoo wa kafara :
    1.Hakuwa mmoja wao,in terms ya kucheck mchezo mzima.
    2.Aliropoka sana to the extent ya kuwaingiza Akina Bank Moon kwenye issue hii.
    3.Alikuwa hana leverage ya kuwa hold masterminds.kumbuka kauli za Kina Muhongo & Maswi kuwa " wakiwajibishwa ardhi ya nchi itachimbika ".
    Kwakifupi mama T inabidi atafute shughuli nyingine ya kufanya kwani maisha yake politically ndio yameishia hapa. Kwa kuwa ameshaonekana ni liability na mchezo game mzuri.

    ReplyDelete
  7. Tatizizo sio maprofessor. Tanzania ni nchi ya kula. Ukipewa nafasi unakula. Cha msingi tu hakikisha hukamatwi. Ukikamatwa utaadhibiwa sio kwa sababu umeiba, bali ni kwa sababu umefanya uzembe ukakamatwa.

    ReplyDelete
  8. Pole Prof Tibaijuka. They say politics is a dirty game.

    ReplyDelete
  9. Huyu mama hakula na wazee nini? Hayo ma press conferences etc ilikuwa ujanja tu, this is really a big scandal, I hope she is ok - counselling may help!

    ReplyDelete
  10. Sawa ameombwa kujiuzulu ili nafasi yake apewe mtu mwengine.Je vipi hizo pesa za uma alizopewa atazirudisha!!?Ni sawa Mr president amemfuta kazi huyu mama lakini pia tunataka tuone pesa zinarudi pia!!!sio kuleta janja ya nyani hapa!!!!

    ReplyDelete
  11. Nakumbuka sakata hili lilipotokea kuna mtu moja alisambaza mitandaoni kumshauri mama T.bora ajiuzulu kulinda heshima yake,badala yake prof.T akaitisha mkutano wa wanahabari ndipo akajivuruga kabisa

    ReplyDelete
  12. masikini mama tibaijuka,kukili kwake kumemweka msalabani.
    Any way njoo nyumbani bukoba tuanze miradi ya kuweka senene katika makopo na pombe la lubisi

    ReplyDelete
  13. This is very serious stuff, from a very senior Cabinet Minister to a backbench na labda kwenda jela. Ana pension ya UN, bora akimbilie overseas na asahau yote hayo.

    ReplyDelete
  14. Raisi amemuomba Prof T atupishe tumteuwe mwingine. Technically ombi linaweza kukataliwa. Inatakiwa itumike lugha sahihi inayoonyesha nguvu ya madaraka na maamuzi. Vinginevyo inakuwa kama vile prof T ananyenyekewa na kubembelezwa aachie ngazi.

    ReplyDelete
  15. Mdau hapo juu umekosea. Mama Tibaijuka amefanywa kafara kwa sababu ya uzembe wake. Amefanya uzembe akajulikana amepewa pesa. Yeye alifungua account kwa jina lake akawekewa pesa.... Huu ni ushahidi tosha wa uzembe. Wenzake wajanja walibeba pesa cash kwenye mifuko ya rambo na magunia. Kumbuka hapa Bongo mtu huadhibiwa sio kwa sababu ya kuiba, bali utaadhibiwa kwa sababu umefanya uzembe ukakatwa.

    ReplyDelete
  16. She can go and live overseas, they have finished her in all aspects of life.

    ReplyDelete
  17. Politics is a dirty game? Yes, she played dirty and got what she deserved. Look here is a person who in her career has been quick to judge and chastise others. Now she received One Million US dollars and hid it to authorities until the scandal broke out!!

    And anyone out there is claiming she was made a scapegoat? Please! What happemed ethics if not common sense? Thanks JK. You didi the right thing, if not too late!!

    ReplyDelete
  18. Nani kasema hela alizopewa ni za umma? Hata akirudisha anarudisha kwa Rugemalira.

    ReplyDelete
  19. Duh Mama T. kaza buti. hela nyingi hizo. Tulia tuli, kula hela yako. Si umelanduliwa? Hizi hela zitakufikisha uzeeni na uaziacha ni nyingi mno.

    Usihofu TZ hamna walio serious. Hutafanywa kitu zaidi ya kukufukuza kazi...Si unajua mnalindana? wewe umetolewa kafara tu.

    Wajinga ndo waliwao

    ReplyDelete
  20. Pole mama T. Kiburi chako cha kuita press conference kimekuacha kwenye mataa sasa. Ona wenzio waliokaa kimya wamebaki. Lakini cha mzinga sasa kaa kimya, sisi watanzania tunasahau haraka, mwakani nunua helikopta za kuzunguka nchi mzima kuomba uraisi kwa nguvu mpya, nia mpya na uwezo mpya. Tuambie sisi watanzania kwamba huwezi kuomba tena kwa sababu unajua hela ya kukutosha sasa. Mungu azidi kukuongezea akili za kuendelea kutunyonya

    ReplyDelete
  21. Baada ya kusikiliza hotuba ya mheshimiwa Raisi bado nina maswali yafuatayo:
    1.Ni kwanini serikali haikumchukulia haikumchukulia hatua IPTL kwa kukwepa kulipa kodi Tax evasion ?alichosema Raisi kuwa TRA wako kwenye mchakato wa kukusanya hio kodi ni recovery process.Ninavyo fahamu kukwepa kodi ni kosa la jinai na mara nyingi TRA wanapaswa kotoza penalties juu ya kodi husika.
    2.Kwanini Serikali haikufatilia hukumu ya kesi ya Tanesco dhidi ya IPTL,ambayo Tanesco walishinda.Na ushindi huo ungeiwezesha serikali kurecover Pesa nyingi za ongezeko la tozo.Mpaka sasa hakuna mtu anaongelea hilo.
    3.Kwakuwa kulikuwa na ukwepaji wa kodi nivipi Waziri wa fedha na kamishna wa TRA hawawajibiki kwa uzembe?
    4.Nivipi mheshiwa raisi anaruhusu watuhumiwa kuendelea kufanyakazi wakati uchunguzi dhidi yao ukiendelea?

    ReplyDelete
  22. Let them use their money, sio za umma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...