JINA la Rose Muhando ni mojawapo ya majina yanayofanya vizuri katika muziki wa Injili barani Afrika  hasa kutokana na uwezo wake jukwaani pindi anapofikisha uinjilishaji kwa waamini na mashabiki mbalimbali.
 
Muhando ni mzaliwa wa kijiji cha Dumila, wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, Tanzania, Afrika Mashariki na ni mwimbaji wa nyimbo za injili kwa lugha ya Kiswahili ambaye umahiri wake awapo jukwaani umefanikisha kutambulika barani Afrika. 
 
Rose atakayepanda jukwaani kuanzia Desemba 25, Agosti 3 mwaka huu alizindua albamu yake Kamata Pindo la Yesu yenye nyimbo za ‘Facebook’, ‘Bwana Niongoze’, ‘Wewe Waweza’, ‘Usiniache’, ‘Nibariki na Mimi’, ‘Usivunjike Moyo’ na ‘Kwema’. 
 
Awali Rose kabla hajawa Mkristo alikuwa Muislam na ni mama wa watoto watatu. Alimpokea Yesu Kristo pale alipokuwa anaumwa na yuko kitandani akiwa na umri wa miaka 9, aliugua kwa muda wa miaka mitatu na baadae alipona na kubadili dini na kuwa Mkristo.Rose alizama kwenye muziki katika kwaya iliyoko Dodoma na alikuwa mwalimu wa Kwaya katika kwaya ya Dodoma St. Mary’s katika kanisa la Kianglikana la Chimuli.
 
Januari 31 mwaka 2005, Rose Muhando alizawadiwa tuzo ya Mtunzi bora wa nyimbo za Injili, Mwimbaji Bora na albamu Bora ya Mwaka. Tuzo hizo zilitolewa katika Tamasha Tanzania Gospel Music Awards, 2004.Desemba mwaka 2005 alihudhuria katika tamasha la Nyimbo za Injili katika kusaidia kuchangia kwa watoto na wajane Dar es Salaam ambapo alitekeleza ipasavyo uchangiaji huo.
 
Februari 2011, Rose Muhando alisaini mkataba na Mult Album Recording Deal na Kampuni ya Sony Music ya Afrika Kusini. Kusaini huko kulitangazwa katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Tanzania na hiyo ni mara ya kwanza kufanyika Afrika Mashariki.

Baadhi ya albamu za Rose Muhando ni:
1. Mteule uwe macho, 2004
2. Kitimutimu, 2005
3. Jipange sawasawa, 2008
4.Utamu wa Yesu 2012
4.Kamata Pindo la Yesu 2014

Tuzo alizopata

2005 -Tanzania Music Awards: Mwimbaji Bora wa Kike Nyimbo za Dini (“Mteule uwe macho”) 
2009 - Mwimbaji Bora wa Nyimbo za Injili
2008- Alitunukiwa tuzo nchini Kenya ya Mwimbaji Bora wa Injili Afrika

Amewahi kuzawadiwa kitita cha Sh200,000 na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bint Mungu akuzidishie. Ikiwa watumia vipaji alivyokupa Mola wako kuendeleza kazi zake hapa ulimwenguni.Nasikia ulikuwa muislam, nakuomba ukumbuke kuwa islam means submission to the will of God and being submissive to His laws.Its the same God, we just approach His kingdom from different routes

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...