SHULE ya watoto wenye ulemavu ya Buhangija Jumuishi inakabiliwa na changamoto kubwa zinazofanya maisha kwa watoto hao kuwa magumu.
Miongoni mwa changamoto hizo ni kukosekana kwa huduma za matibabu, walimu wa kutosha na mabweni.
Hayo yamebainika wakati wa ziara fupi ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues.
Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi, ndiye aliyeelezea ugumu uliopo katika shule hiyo yenye wanafunzi 209 wenye ulemavu wa aina mbalimbali.
Alisema shule hiyo yenye walemavu wa aina tatu wa kusikia, ngozi na wasioona inakabiliwa pia na lishe duni ambayo haimpi kijana nafasi ya kuendelea, kwani wanakula mlo wa aina moja na kidogo.
Shule hiyo ambayo awali ilikuwa inawapokea wanafunzi wasioona sasa inapokea walemavu wa ngozi kutokana na hofu iliyokuwa inalikumba taifa ya mauaji ya albino.
Aidha mwalimu huyo alisema kwamba wameiomba serikali kuwa na muuguzi na daktari katika makazi hayo lakini mpaka sasa hawajapatiwa kutokana na wao wenyewe kutokuwa na uwezo wa kuwalipa.
Alisema kutokana na rika mbalimbali na tatizo la walemavu wa ngozi shule hiyo ambayo sasa imegeuzwa kuwa makazi inastahili kuwa na daktari na mabweni yaongezwe.
DSC_0191
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ( wa pili kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga (hawapo pichani) alipofanya ziara fupi akiwa safarini kuelekea jijini Mwanza akiwa ameambatana na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias (wa pili kulia). Kulia ni Mkuu wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi.
Aidha mwalimu alisema walimu kwa ajili ya viziwi hawatoshi.
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, amesema ameyaona mazingira hayo na kuahidi kushirikiana na marafiki na mamlaka nyingine kuboresha mazingira ya kituo hicho.
Alisema kwamba amefurahishwa kuwapo katika kituo hicho na kuona namna wanavyoweza kusaidia sehemu hiyo ya jamii kutojisikia upweke.
Akizungumza na watoto hao walimwambia kwamba wana changamoto ya nguo, vitanda, vitabu na mahitaji mengine ya lazima kama watoto na wanafunzi.
DSC_0177
Baadhi ya watoto wanaosoma shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani Shinyanga wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (hayupo pichani).
DSC_0201
DSC_0222
Mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Loreto mkoani Shinyanga Beatrice Leme anayelelewa kwenye kituo hicho kutokana na kukithiri kwa mauaji ya walemavu wa ngozi mkoani humo akimwelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa niaba ya wanafunzi wenzake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefanya ziara fupi shuleni hapo.
DSC_0306
Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wakicheza mpira kwenye mazingira salama shuleni hapo kutokana na hofu iliyokuwa inalikumba taifa ya mauaji ya albino.
DSC_0308
Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi akimtambulisha mtoto Erick mwenye ulemavu wa ngozi kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) aliyefanya ziara fupi kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu (mahitaji maalum).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mungu awabariki watanzania hawa walioko shule hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...