NA CHALILA KIBUDA WA GLOBU YA JAMII.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka amesema kuwa hawezi kujiuzulu katika nafasi  ya uwaziri kutokana fedha ya Tegeta ESCROW. 
Akizungumza  na Waandishi na Habari mapema leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hoteli ya Hayyat Regency, Profesa Tibaijuka  alisema kuwa udalali wake wa  fedha hiyo ni kwa ajili ya wanafunzi katika shule  za Taasisi ya  Barbo Johansson  Girls Education Trust, na kwamba fedha aliyoipata ni  Bilioni  Tshs. 1.66 ambazo zilitoka katika kampuni ya James Rugemalira kama msaada kwa shule hiyo.
Alisema kuwa fedha hiyo kuingia katika akauti yake binafsi ilitokana na masharti ya mtoa msaada ndugu James  Rugemalira  ambaye alitaka fedha hiyo iingie katika akauti ya Benki ya Mkombozi. 
"Nikijiuzulu hata Rais Jakaya Kikwete atanishangaa kwani fedha nilizopata ni za shule na kwa ajili kukomboa elimu nchini  hasa kwa watoto wa kike kutokana na wazazi wengi kutoweza kumudu gharama za shule’’alisema.

Alisema kuwa udalali wake ni kutafuta  fedha kwa ajili ya elimu nchini ambapo, alidai hata Mwenyekiti wa Makampuni  ya IPP  Dkt Reginald Mengi alitoa sh.milioni 248 kwa ajili ya msaada wa shule hiyo.

Profesa Tibaijuka  alisema kuwa  wananchi watambue kuwa yeye ni mstaafu wa Umoja wa Mataifa hivyo hawezi kufanya hivyo na kama angetaka fedha hiyo angeweza kufuata hata katika shule na kuchukua.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo.
 Sehemu ya Waandishi wa Habari waliofika kwenye Mkutano huo ulioitishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 63 mpaka sasa

  1. anachotakiwa kujibu ni kwa nini hela nyingi kama hiyo iliyoingia kwenye account yake binafsi Hakuiweka wazi kwenye kamati ya maadili ya viongozi na ikajulikana kwamba ilikuwa ni mchango wa shule yake.KINACHOTAKIWA PIA ARUDISHE BAADHI YA HELA,HAIWEZEKANI HELA YOTE IKACHANGIA ELIMU KWENYE SHULE MOJA TU,AMBAPO TUNA SHULE AMBAZO HAZINA MADAWATI NA VITABU HAPO NCHINI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Majibu ya huyu mama yanasikitisha

      Delete
  2. Pili ajiulize kama Bw Mengi anatoa milioni 280 Tshs huyo Bw Rwegemalira anapata wapi uwezo wa kutoa Tshs 1.66 bilioni? yeye kama Mchumi hakuweza ona hiyo fedha haikuwa halali kwa kuzingatia kipato cha mtoaji? Huku ni kudhalilisha taaluma yako kama Mchumi na unapaswa kujiuzulu kama Rais Mstaafu alivyofanya kipindi cha mauaji Shinyanga alipokuwa Waziri wa mambo ya ndani

    ReplyDelete
  3. WAANDISHI WA HABARI WAPO PICHANI....

    ReplyDelete
  4. Kama hutajiuzulu na Rais akakuondoa si itakuwa aibu zaidi? Umewa disappoint women and young girls who had aspired to be like you and Migiro. Given kwamba umefanya kazi UN ambako maadili yako katika kiwango cha hali juu, hili ndio linatushangaza zaidi wengi. Hoja ya elimu uliyoiweka kama sababu za kupokea m 280 plus 1.66 Billion nakubaliana nayo kuwa ni ya msingi, only kama ingefanyika katika proper channels and procedures na pia kama ingelenga wahusika stahili. Sielewi kwa nini all that money went to just one single school badala ya kutumika kusaidia shule nyingi tu za kata na nyinginezo ambazo kuna uduni mkubwa wa vifaa vya elimu na maabara. Hiyo shule ya kuhitaji over Tsh 1.9 billion equivalently over 1 million USD katika mazingira ya Tanzania, hii shule ni ya aina gani hiyo na inawasaidia wanafunzi wepi hao hadi kuhitaji pesa zote hizo? Ningekuelewa kama hizo pesa zingetumika katika shule 100 za kata, lakini sio shule hiyo moja. Viongozi hujiuzulu sio tu kwa sababu ya kufanya makosa, hujiuzulu pia kama kauli ya wengi inataka wajiuzulu. Wahenga walisema wengi wape. Pengine wewe huoni sabababu kwa sababu umekuwa blinded na interests zako, lakini wenzako wanaziona ndio maana wanakutaka ufanye hivyo. Kukataa kujiuzulu ni kiburi tu, nothing else.

    ReplyDelete
  5. Prof hapa tatizo lipo na linaonekana kutokana na huu mgao ulivyo fanyika...
    Inaonekana kuwa kuna 1.6bl zimelipwa kwawatu kama wawili.
    kuna 40.4mlioni kama tatu na nyingine zinazo fuatana hivyo.
    Inawezekana ikawa wewe sio mwizi lkn umeingia kwenye tata kwahiyo jiunzulu tuu.

    ReplyDelete
  6. Umetuaibisha sisi sote tuliokuwa tuna-aspire Kiwia kama wewe. Ndio, umefanya IN, kwa nini hukuweza kuandika a simple proposal ya kuwasaidia akina mama (watoto wa kike ulisema?). UNFPA au hata UNDO wangekusaidia. Je utaweza kutuonyesha proposal uliyomwandikia Lugemarila?. Zaidi ya kukusaidia wewe alipeleka wapi tena kiasi kikubwa hivyo kusaidia shule zingine? Au hii danganya toto? Mama achia tu madaraka - easy, la sivyo, utadissapoint wengi zaidi, na reputation yako itaangamia 4ever
    Mungu ibariki Tanzania, Mungu wape adhabu wale wote wanaoliibia taifa letu

    ReplyDelete
  7. Mheshimiwa waziri mama Tibaijuka, nataka uelewe wazi kwamba: Michango mikubwa kwa taasisi yeyote ya kijamii hutolewa hadharani na hutangazwa kwenye vyombo vya habari ili kuujulisha uma na kumpa heshima mtoaji.

    Sasa, wewe umefungua account ya binafsi haraka haraka maalum kwa ajili ya kupokea hizi pesa. Kwani shule haina account??? Halafu umekaa kimya mpaka moto ulipowaka bungeni ndio unajitokeza na kuleta hadithi ya mchango wa shule. Hivi unafikiri watanzania million 50 wote ni wajinga, ni wewe tu mjanja???

    Mama waziri Tibaijuka, kubali makosa na ujiuzulu. Kutunza heshima yako ni kuonyesha wananchi kwamba umeyaona makosa yako na umechukua hatua za kuachia ngazi. Ukifanya hivyo wananchi watakusamehe na watakuheshimu. Ukiendelea kujitetea ni kama vile unawafanya wananchi wote kuwa ni wajinga na kwamba hawaoni makosa uliyoyafanya.

    ReplyDelete
  8. Mheshimiwa waziri Tibaijuka. Usiogope kukubali makosa, na wala usiogope kuomba msamaha. Stand firm, accept your mistake, take responsibility and apologize. If you take these steps, you will come out stronger than ever.

    Kwa kweli hata sisi wananchi wa kawaida tunaona wazi kuna makosa makubwa yaliyofanyika hapa. Umefungua account ya binafsi maalum kwa ajili ya kupokea Sh 1,600,000,000. Kwanini ufungue account binafsi maalum kwa ajili ya kupokea hizi pesa?? Kwani wewe mwenewe huna acconut nyingine?? Kama kweli ulikuwa ni mchango wa shule, kwani shule haina account?? Na ni kwanini hukutangazia uma kwamba umepokea hilo fungu na kwamba hizo pesa madhumuni yake ni nini.

    Mimi ni mwananchi wa kawaida lakini ninaona wazi hapa kuna matatizo makubwa. Kuendelea kungangania uongozi wa ofisi ya uma katika hali ya namna hii kasfa kubwa kwa wananchi.

    ReplyDelete
  9. Mboba hiyo shule anayosema imepewa msaada ada yake ni kubwa sana kulinganisha na shule nyingine za binafsi wala haihitaji kuchangiwa ili kuiendesha. Haya tukubali umepewa huo mchango kwa ajili ya shule, je dili la ESCROW lisingebumbuluka ungesema ni za shule au ungabana kimya?

    Na kama huyo mtoaji alikulazimisha kulipa hiyo pesa kupitia Bank ya Mkombozi kwanini shule ilishindwa kufungua akaunti yake kwenye hiyo Bank ukizingatia ukubwa wa kiasi cha pesa? Kwani shule hairuhusiwi kufungua akaunti nyingine inapobidi? Kwani masharti ya shule kufungua akaunti ni magumu kiasi gani mpaka wakashindwa kufungua akaunti hapo Mkombozi Bank? Usitufanye hatukwenda shule na hatuna akili za kuchanganua mambo?

    Cha ajabu kama Kiongozi huruhusiwi kuchukua msaada au zawadi ya aina yoyote inayozidi shs 50,000 bila kutoa taarifa kunakohusika.

    Mbaya zaidi mpaka leo hujasema kuwa sio wewe tu peke yako uliyepewa pesa na James Rugemalira hata Binti yako Kemilembe pia amepata mgao mkubwa tu, je na yeye ni kwa ajili ya shule? Au hizo mishe mishe zake za mishen Town?

    ReplyDelete

  10. Kosa la kwanza ni kuchukua hizo pesa kwa account yake...kama ilikuwa ni sharti kwa nini akufungua trust fund yake...for accountability purpose..
    aonyeshe bank statement tuone pesa zilivyotoka kwake kwenda kwa shule hiyo...na pili hiyo shule inyoshe pesa zimeingia na matumizi yake to Zero...

    Auditors wa serikali kazi hiyo..tuelewesheni....

    ReplyDelete
    Replies
    1. That's itoe mchanganua na vielelezo jinsi pesa ilivyotumika ,1.6 billion for a single school? You got to be kidding me

      Delete
  11. kuna haja ya viongozi wa serikali kufundishwa PUBLIC SPEAKING....sijawahi kuwaza uprofessor ni rahisi namba hiyo kwa akili kama hizi.

    tunashukuru kikwete.

    ReplyDelete
  12. I am sorry to say it is shameful kwamba Prof. haonin tatizo katika hili. This is the caliber of leaders we have? What a shame. Kama mdau hapo juu kweli umetuangusha wanawake wote na watoto waliotaka kuwa kama wewe. kumbe after all wanaume na wanawake wote wakipata madaraka hawana nguvu za kukataa vishawishi na kusimamia maadili bora. Prof I am so disappointed in you and your shameless courage. Sad day for women in our country

    ReplyDelete
  13. Fedha zilipoingizwa kwenye account tayari zilikuwa male yake,,si za shule? baada ya kuzitoa kuingiza katika shule ndio zikawa za shule kwa maana hii alipewa fedha za umma zikaingizwa katika akaunti yake ni Utakawitishaji wa fedha chafu Kuelekea katika usafi wa matumizi

    ReplyDelete
  14. Mheshimiwa raisi, ninakuomba ufanye kile serikali ya China inachofanya. Mtu yeyote atakayeonekana kushiriki kwenye vitendo vya rusha na ufisadi achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria bila kujali cheo au wadhifa wake. Inakuwaje fedha nyingi za uma kuingia mifukoni mwa viongozi waliokabidhiwa madaraka ya kuuongoza uma??? Hospitali hazina dawa, mashuleni hakuna vifaa, wananchi wa kawaida tunahangaika hata kupata nauli ya daladala!!

    ReplyDelete
  15. Raisi alikuwa amelazwa anapata matibabu Marekani, huku nyumbani viongozi wa serikali wa ngazi mbalimbali wakajipaga kusuka mission ya kuchangamkia zaidi ya shillingi billion 300. Inasemekana pesa imechukuliwa kwenye magunia, mifuko ya rambo, vikapu, na account binafsi zilizofunguliwa chap chap. Sasa raisi amerudi nchini, ninaamini nyie wote mliohusika matumbo ni moto.

    Mimi natoa ushauri, kama ulihusika basi jisalimishe na omba msamaha kwa wanannchi. Na hiyo pesa rudisha.

    ReplyDelete
  16. Waziri Tibaijuka, ni afadhali ungekaa kimya kuliko kujitetea hadharani. Huwezi kuudanganya uma. Mwishowe ukweli utajionyesha tu.

    ReplyDelete
  17. Jamani mama T what has Umoja wa Mataifa got to do with this?

    Hakuna uhusiano na hilo sakata la hizo fedha.

    Nakubaliana na mtoa hoja namba tano kwamba laiti fedha hiyo ingetumika kwa shule za kata katika jimbo lako la uchaguzi basi tungeweza kukusamehe. Siyo hiyo shule ambayo school fees yake ni mhhhhhh!

    Endelea kujichanganya tu mama sisi hapa tunakusubiria kujiuzulu kwako kwa hamu kubwa.

    ReplyDelete
  18. 1. Kwanini pesa hii iingie kwenye personal account? c'mmon lady you are educated and smart, you know better.
    2. Kwanini iende kwenye shule moja?
    3. Kwanini usitoe mchanganuo na risiti za matumizi ya hiyo fedha kutoka huko "shuleni" ilikopelekwa?
    4. Mama umebainika! Aibu! JIUZULU!

    ReplyDelete
  19. Mimi katika pitapita zangu kwenye mitaa ya Dar, moyo wangu unauma sana ninavyoona jinsi umaskini ulivyokuwa mkubwa. Mimi mwenyewe nahangaika lakini ninavyoona mama amebeba mtoto amekaa pembeni ya barabara anauza mandazi au vitumbua kweli roho yangu inauma. Na ukifanya utafiti kidogo utakuta huyu mama kwenye ndoo yake kuna mandazi 20 tu. Hata akifanikiwa kuuza yote, ni shida tupu. Na huyu mama mzalendo akienda hospitali anaambiwa, "mama dawa hamna"........

    Swali langu kwa viongozi wa juu wa uma, hivi kweli hamuoni shida tunazopata wananchi??? Tunaposikia kuhusu wizi wa pesa za uma zaidi ya shillingi billion 300, hii inatuumiza sana sana sana.

    ReplyDelete

  20. Mimi nadhani bora angekaa kimyaa kwa kweli !

    ReplyDelete
  21. Only in Tanzania --> utakuta matuta ya barabarani kwenye major highway.
    Only in Tanzania --> Shule za serikali hazina hata madawati.
    Only in Tanzania --> Mji mkubwa wa Dar ni mchafu kuliko miji ya mikoani.
    Only in Tanzania --> hospitali hazina dawa, maji safi hakuna, lakini viongozi wa uma wanachangamkia pesa za wananchi zaidi ya Sh 300,000,000,000.
    .........................
    ........................
    Ongeza mengine...

    ReplyDelete
  22. Hiyo inaitwa " money laundering " , hiyo pesa imeingizwa shule ili kuifanya ionekane ni pesa halali/ safi na kuwa ni pesa ya msaada kwa shule. Kama ni mtu unayejitolea kuinua elimu nchini kwa nini pesa yote iingie kwenye shule moja?, hiyo pesa inahitajika hapo shuleni kwa matumizi gani?, hiyo pesa ni nyingi mnoooo kwa shule moja. Kwani hakuna shule nyingine zinazohitaji msaada?, ni shule ngapi nchini bado zinahitaji madawati na vitabu?, ni shule ngapi bado zinahitaji maabara?, maktaba?, vyoo na huduma za maji?. Kushikilia msimamo huo kunaonyesha ni jinsi gani huyu mama anawafanya wananchi wa tanzania kuwa ni mambumbumbu ambao watakubali uongo wowote atakaotoa ukichukulia pesa iliingia kwanza kwenye akaunti yake binafsi halafu ikapelekwa shule ili kusafishwa..JIUZULU KWA HESHIMA NA UADILIFU MAMA!!!!

    ReplyDelete
  23. Majibu ya huyu mama yanaaibisha sana. La msingi ni kuwa shule iliyojengwa kwa hela za walipa kodi ni MALI YA UMMA.

    ReplyDelete
  24. Mama Waziri Tibaijuka, hivi huoni aibu kujitetea hadharani? Yaani wewe unaona watanzania millioni 50 ni wapumbavu tu!! Tafadhali ona makosa yako na ujiuzulu na tena uombe msamaha. Na hiyo pesa urudishe yote.

    You are one person I admired the most. I am so dissapointed. Ningekuwa na nafasi, I swear to God, ningekuchapa viboko. Nilikuwa nina imani kwamba wewe ni mkombozi, kiongozi wa kutegemewa na wa kutoa mfano kwa kizazi kinachokuja. What happened to you?? Tafadhali mama waziri, okoa ile heshima iliyobaki, JIUZULU NA OMBA MSAMAHA KWA RAISI NA KWA WANANCHI.

    ReplyDelete
  25. Mama waziri Tibaijuka, nenda Ikulu sasa hivi uwasilishe barua yako ya kujiuzulu na umuombe raisi msamaha. Kesho asubuhi itisha kikao na waandishi wa habari ukiri makosa na uwaombe wananchi msamaha.

    Tafadhali mama waziri, chukua hii nafasi uweke historia ya pekee katika taifa letu la Tanzania. Kubali makosa hadharani, omba msamaha and move on. You will come out stronger than ever before.

    Mama Tibaijuka, wewe ni kiomngozi mwenye kipaji na uwezo mkubwa. Sasa onyesha Taifa kwamba una ujasiri wa kusimama mbele ya wananchi na kukubali makosa na kuomba msamaha. Watu wengi hufanya makosa katika maisha, lakinini ni wachache wenye busara na ujasiri wa kusimama hadharani na kukubali makosa na kuomba msamaha.

    Wananchi wengi wamekasirika zaidi kwa sababu wewe uliyekuwa tegemeo la wengi umetuangusha.

    ReplyDelete
  26. Mama hapa umenasa kwenye mtego wa panya. Kubali tu kwamba umekamatika. Unajitetea nini wakati umenaswa kwenye mtego wa panya? Huna pa kujificha, umebanwa na mtego, na umma wa watanzania unashuhudia, na wengine kushangilia.

    Lakini usikate tamaa, its not the end of the world. Hali ngumu kama hii ni nafasi muafaka ya kuonyesha uwezo wako wa kuongoza jamii. Na ili kuonyesha busara na uwezo wako wa uongozi, JIUZULU, OMBA MSAMAHA KWA RAISI, NA OMBA MSAMAHA KWA WANANCHI.

    Wewe ni muwakilishi wa raisi wizara ya Ardhi, na ni mtumishi mkuu wa uma. Sasa umenaswa na shutuma kubwa...... Unapoendelea kujitetea kwa kosa linaloonekana wazi ni kama vile unawakashfu wananchi na Raisi. Tunza heshima yako mama. JIUZULU.

    ReplyDelete
  27. Shame on you Professor. The more money you have the more money one needs! For what? And why get it the way you GOT it? You should step down right away! We do not have any faith in you at ALL mama! Sorry. I used to respect you a lot, but I am done! Sorry!

    ReplyDelete
  28. Raisi alikuwa kwenye matibabu Marekani, wao wakajipanga kuchangamkia pesa ya wananchi Shillingi billion 300 (about US $ 200 million). Mimi naona kama vile walifikiri Raisi hatarudi. Yaani hii ni kashfa na dharau kwa wananchi. Namuomba Raisi achukue hatua ambazo itakuwa ni mfano na historia kwa Taifa letu.

    Namuomba Raisi awaondoe madarakani wote waliohusika, na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria. Namuomba raisi awaite watanzania walio waaminifu na wenye uchungu na taifa letu kokote waliko duniani waje wachukue nafasi zitakazoachwa wazi. Tafadli mheshimiwa raisi, fanya shake-up ambayo haijawahi kutokea katika taifa letu.

    Mheshimiwa raisi, tafadhali leta mapinduzi ya uongozi na maadili utusaidie kuuondoa huu uovu uliohalalika wa kuiba pesa za wananchi, wakati hospitali za umma hazina hata dawa. Wewe ndio tegemeo letu mheshiwa raisi. Ninaamini wananchi walio wengi wako nyuma yako mheshimiwa Raisi.

    ReplyDelete
  29. Mtu mzima akivuliwa nguo huchutama,hainami. Umejiaibisha sana prof.

    ReplyDelete
  30. Hivi kweli hizi ndio akili za uProfessa? Amazing. Kumbe wakati mwingine shule haisaidii. Hata hao wadau hapo juu wanaosema akiomba radhi atasamehewa hawamsaidii. Hivi ndivyo tunavyojenga tabia ya kuvumilia uvunywaji wa Maadili na Sheria.

    Kuna swali kubwa sana la kimaadili. Ile tu kwamba hadi sasa bado ni sehemu ya Serikali yetu inaonyesha tusivyokuwa na maadili. Wakati mwingine ile kutuhumiwa tu - rightly or wrongly inatosha kusema naomba nijiondoe nisiwe mzigo kwa Serikali ama Nchi yetu. Huo ndio utawala bora. Sasa hili nalo professa akasomeshwe?

    ReplyDelete
  31. Mheshimiwa Raisi, hii nchi inahitaji your action. Kila kitu kina turning point. Katika kashfa zote za kifisadi ndani ya Tanzania, mimi naona hii imetufikisha kwenye tipping point. Kumbuka kwamba Dar haia maji, mahospitali ya umma nchi nzima hakuna dawa, nk, nk, ... Halafu viongozi wakuu wa umma wanaiba pesa ya wananchi Sh billion 300. Yaani hii nchi inahitaji overhaul. Mheshimiwa raisi shusha injini, vifaa vibovu vyote tupa. You have the support of Wananchi Mr. President.

    ReplyDelete
  32. Nasikitika wote mnacomment kwa emotions na sio uhalisia. Mbona hamuongelei kiasi alichochangiwa na mengi kama kilistahili kutolewa au la? Mbona hela alizochanga mzee mengi zinaonekana sio tatizo? Pili Ni wapi ripoti ya mkaguzi WA serikali ilimtaja Prof tibaijuka? Kwa nini hamliongelei hilo? Alafu inabidi Pia mjiulize Ni wapi wameweka ukomo WA kuchangia kwenye msaada? Kuna sheria ya ukomo wa kuchangia?

    ReplyDelete
  33. My serious problem with our leaders, they do not care. Sisi Muhimbili hatuna dawa na nyie mnagawana mabilliooni. Get rid of all the Professors and Drs, hao ndio wanahujumu nchi, they think they can get away with anything.

    ReplyDelete
  34. Prof Tibaijuka, kuna wakati hata janja ya kiprofessor haisaidii. Kama alivyosema mdau hapo juu, sasa hivi umenaswa kwenye mtego wa panya na umeanikwa hadharani. Janja ya kiprofessor hapa haisaidii. Accept you mistakes, take responsibility and apologize. Its the best you can do.

    ReplyDelete
  35. Eti mtu anauliza kwa nini achangie shule yake wakati Kuna shule nyingi hazina madawati. Mbona hamjiulizi kwa nini mtu anachangia harusi Fulani mamilioni alafu hachangii watu wenye shida? Hamna sheria inayomlazimisha mtu kuchangia kitu fulani na vilevile kuchangia ni utashi na roho ya mtu. Alafu waziri kasema walimuomba ruge mchango ndo akachangia. Mbona hili hamlioni? Hizo shule zisizo na madawati zishawai kumuomba ruge achangie na akakataa?

    ReplyDelete
  36. You gotta go and you have to go. Waste of time and space with all these press conferences. You have failed to convince us at all. You never declared the funds, it only came to light becuse of Hon Kafulila. Usitufanye wapumbafu sisi wote.

    Bishops, sheiks, judges etc were all given monies - so tell us what is going on!

    Follow the AG example.

    ReplyDelete
  37. Mama Tibaijuka, wewe mwenyewe unaishi Makongo. Unajua wazi jinsi ambavyo wananchi wa Makongo wanavyopata shida ya maji na barabara. Unajua wazi jinsi ambavyo Makongo nzima hata kituo cha polisi hakuna. Unaona kila siku jinsi ambavyo wananchi wa kawaida wanavyohangaika. Hivi inakuwaje mtu katika nafasi ya juu kama uliyokuwa nayo kujiingiza kwenye kashfa yenye utata kama hii?? Hata ukiwa na mabillioni ya shilingi wakati jamii inayokuzunguka haina hata maji au barabara, hayo mabillioni yatakusaidia nini?.

    ReplyDelete
  38. Prof Tibaijuka. You have let us down, and I think Wananchi feels betrayed and let down. But I still admire you. I just hope you will what is right. Good luck prof.

    ReplyDelete
  39. Michango mikubwa kwenye taasisi za kijamii hutolewa hadharani na hutangazwa rasmi kwa umma. Kuna sheria zinazosimamia michango. Ile tu kwamba alienda kufungua account binafsi rasmi kwa ajili tu ya kupokea hizo pesa ni tatizo tosha. Huyu ni waziri kiongozi mkuu wa serkali. Huyu mama ajiuzulu akae pembeni aachie vyombo vya dola vifanye kazi yake kuangalia uhalali wa yote haya.. If she is innocent it will come out, and if she is guilty she should go to jail. Sheria ifuate mkondo wake.

    ReplyDelete
  40. Kasha dhidi yako ni nzito mama waziri Tibaijuka. Mimi naona cha busara kufanya ni wewe kukaa pembeni, JIUZULU, waachie vyombo vya dola wafanye kazi yao kwa misingi ya sheria za nchi. Kama huna hatia jina lako litasafishwa. Hakuna sababu ya kungangania wakati wananchi wanaonekana kupoteza imani na wewe. Na pia viongozi wengine wote waliotajwa kwenye hii kashfa inatakiwa WAJIUZULU, waachie vyombo vya dola vifanye kazi yake.

    ReplyDelete
  41. Ni Professor huyu, check the number of waandishi wa habari- kibao wamejazana kusikiliza mulenda. Uongo Uongo mkubwa. Very sad story.

    Usipojiuzulu basi utafukuzwa. Kujiuzulua ni kufukuzwa kwa heshima.

    ReplyDelete
  42. It is very sad for our country. Lakini kutegemea na hatua ambazo Raisi atachukua, it might be a turning point for our country for a better future. Tunasubiri kuona maamuzi ya Raisi.

    ReplyDelete
  43. Maana ya kuwa kiongozi wa umma ni nini? Mimi nafikiri jamii yetu ya Watanzania tumeshapumbazwa. Kwa miaka mingi tumeona viongozi wa juu wa umma wanajinufaisha kwa kiwango kikubwa na tunaona ni sawa tu!! Kashfa nyingi zimejitokeza, watu wamepoteza wadhfa au kuhamiswa wizara, na wengine kesi kwenda mahakamani, lakini hakuna jela kwa wale vizito wa uhakika -- wananchi wanaona sawa tu. Dar maji hamna, shule vifaa hamna, haspitali dawa hakuna, halafu viongozi wa umma wanaiba Sh 300,000,000,000???? Tuendelee tu kuona ni sawa tu? Sasa hivi Tanzania viongozi wengi wa juu ndio matajiri wakubwa, hiyo pesa wanatoa wapi? Mishahara yao tunajua? Hili sakata la Escrow litatoa tu mwanya kidogo kutuonyesha wananchi wa kawaida kile kinachoendelea. Tujiulize, kuna mangapi yanakwenda chini chini bila kufahamika???? Tuamke, na tumuombe Raisi achukue hatua kali.

    ReplyDelete
  44. Huyo aliyesema only in Tanzania...

    It is only in Tanzania Professors run away from teaching to go to Politics.... Anyone with an idea as to how many professors in Mr. Kikwete's cabinet? Halafu tunasema shule na vyuo havina waalimu wa kutosha? Kuna nini kwenye politics? Pesa za R-u-s-h-w-a? Rushwa ni ADUI was haki. Sitapokea wa kutoa Rushwa!! Mama hii hukuisoma na kuiimba wakati ukienda shule? Mama SINA IMANI NA WEWE TENA. Ningekuwa wewe ningetamani dunia ipasuke niikimbie! Pole! Jiondoe. Jiachie....Achia ngazi.

    ReplyDelete
  45. Tanzania peke yake waziri anaweza kuongea huo ujinga na baadhi ya wananchi wakakubaliana nae na wakaendelea kumpa madaraka,kweli inaingia akilini,huo usomi wako ndo unaofanya wananchi wajinga kwa kuongea vitu kama hivyo?hizo hela zote ni chafu kutoka kwa uliekupa na wewe mwenyewe uliopokea,my fellows tanzanian please WAKE UP!!!!!

    ReplyDelete
  46. Inashangaza kuona watoa comment wote wanataka huyu mama ajiuzulu na hii inaonyesha tabia ya ufisadi itaendelea milele Tanzania,mtu akituhumia amekula rushwa inapaswa uchunguzi ufanyike na ikibainika kweli alikula rushwa inabidi ahukumie jela kutokana na makosa yake,mwingine atakuja iba hela Zaidi ya hizo akishtukiwa anajua atajiuzulu na hela anabaki nayo,kazi kweli kweli nchi yangu na tuna safari ndefu sana.

    ReplyDelete
  47. Kama mimi ningekuwa Raisi, mtu yeyote aliyehusika kwenye hii kashfa ya ufisadi angekiona cha mtema kuni. Ningetumia hii nafasi kuleta mapinduzi kwenye uongozi wa nchi. Hata kama ni baraza zima la mawaziri kuondoka ningewaondoa. Ningeleta viongozi wapya, nikikosa viongozi waaminifu kwenye bunge la sasa, ningechukua viongozi jeshini au popote duniani alipo mtanzania. Wale Ambao watadhibitika kushiriki kwenye kashfa wote wangeenda jela kutumikia kifungo kikali na kazi ngumu.

    ReplyDelete
  48. Dawa yenu iko jikoni. Nasisikia mheshimiwa Raisi ameagiza kuni za ziada, vijana wanachochea moto, dawa inakaribia kuiva........

    ReplyDelete
  49. Katika shughuli zangu ninasafiri Tanzania nzima. Kwa kweli ndugu zangu kuna umaskini Tanzania hii ambao huwezi kuuelezea mpaka ushuhudie mwenyewe. Kuna shule hazina madirisha, sakafu ni vumbi, watoto wanakaa kwene mawe. Kuna vijiji hakuna maji, kina mama wanakwenda kilomita kadhaa kuchota maji kwenye madinbwi machafu. Hapa hapa Dar, zunguka tu mitaani uone uchafu ulivyorundikana, maji ya shida, barabara mbovu. Mimi ninaushuhudia umaskini kila siku kwenye safari za shughuli zangu. Sasa ninaPoambiwa kwamba viongozi wa serikali wameiba Sh billion 300 za umma, kwa kweli siwezi kuelewa. Kuna wananchi wanakufa kwa ajili ya kukosa dawa ya Malaria. Sasa hawa viongozi wanaoiba pesa ya umma inatakiwa washtakiwe kwa kosa la mauaji ya umma.

    ReplyDelete
  50. Hii nchi inaitwa Bongoland. Maana yake ni kwamba watanzania wengi tunalala macho tunapiga mahesabu ya Mission za wizi. Yaani ubongo wa mtanzania haulali. Kila mtu kwa namna yake na kila mtu kwa nafasi yake. Juzi polisi kanikamata kosa la gari, kaniambia leta elfu 10 au nikuandikie risiti ya elfu 20. Rafiki yangu kaingiza container, ofisa wa kodi wakachukua mpango wao wakampunguzia kodi. Vijana wa mtaani wanaiba hata alama za barabarni wanauza kama chuma chakavu.

    Sasa ujue kwamba viongozi wa juu wa serikali mahesabu yao ni mazito - ndio hizo billion 300. Na hii ni bahati mbaya tu kwamba habari zimeleak imefahamika. Kuna mission nyingi zinapita chini kwa Chini na hazijitokezi.

    Sasa hivi tuko kwenye nafasi ngumu sana kama taifa kwa maana wengi wetu tunashiriki kwenye haya maovu. Ni nani wa kumnyooshea mwingine kidole???? Wengi wanaolalamika ni ile tu kushabikia kwa sababu hao wa Escrow wamekamatwa. Lakini wewe mwenyewe mlalamikaji kama unaishi hapa Bongo kuna chance kubwa umeshashiki kwenye wizi wa mali za uma kwa namna moja ama nyingine. Umesafiri kikazi ukaongeza siku za safari, ama ukaghushi risiti. Umetorosha ink catridge za ofisini, umeenda shambani kwako na gari ya ofisini kwa mafura ya ofisi, nk,nk. Tutajinasuaje hapa??

    ReplyDelete
  51. Hii ni ishara inayoonyesha kushindwa kujitawala. Na kwa mwendo huu, ukoloni utarudi kwa style mpya, na wananchi wataukaribisha. Yaani ukikumbuka historia baba wa taifa Nyerere na ujamaa wake, na kutaifisha mali za watu, na kuhubiri maadili ya viongozi wa umma, na ....... Sasa hapa ndipo tulipofika. Ni sheria tu za porini zinatawala, dog eat dog, survival of the fittest. Ninyi watu wa chini mlie tu, hili dili la Escrow sio la mwisho. Kuna mengine mazito zaidi yanapikwa. Hii ni nchi ya walaji, ukipewa nafasi unakula mpaka ukoko.

    ReplyDelete
  52. Upeo wa watu kumbe bado ni mdogo Sana. Wapi walisema fedha zililipwa kwa hawa watu wakati raisi akiwa kwenye matibabu US? Inabidi watu mseme ukweli na sio kupotosha humu ndani. Hii blog inasomwa na watu makini na wenye uelewa mkubwa Sana wa mambo.

    ReplyDelete
  53. inahuzunisha sana jinsi maisha yalivyo magumu mtaani halafu mama ana ongea kwa kiburi kua hawezi kujiuzulu eti kujiuzulu ni fashion , pole sana mama Tibaijuka fedha ikikuzidia ndio unaona uko juu ya vichwa vya watu milion 50 huku ukipokea fedha za bila uhalali, Mungu wa mbinguni na awapumzishe viongozi kama wewe ili watanzania masikini wapate nafuu

    ReplyDelete
  54. Mama T, chances are you approached Mzee wa Heinken kwa ajili ya kuchangia shule hatukatai lakini utakua ulijua kwamba amepata hela za escrow hiyo ni wazi,kwa sababu rugemalira ana hela tangia kipindi cha heinken mbona hukumuaproach na Shule yako ni private school na ada yake itakuwa ni kubwa so sidhani kama shule yako ni katika shule ambazo zinahitaji kuomba msaada na ikapata msaada wa 1.6b ambayo hata huku bother kuitangaza kwa umma kwamba umeipokea jamani katika hali ya kawaida mabank,makampuni ya simu yanachangia michango hata ya milioni kumi tu kwa mashule ya kata kwa ajili ya madawati na kila siku tunawaona kwenye vyombo vya uma wakitangaza hadharani leo hii mtu binafsi anachangia 1.6b kwa ajili ya shule inaingia kwenye personal account ya mwenye shule kimya kimya, seriously mimi sioni what is there to justify, na hata kama hukutaka kutangaza kwa uma kuhusu mchango why huku bother kuitangaza kwa shule yako wajue tu kwamba kuna msaada wa 1.6b, je uliita uongozi wa shule yako kutoa news kwamba shule imepewa msaada mkubwa kama huo. Two words ACHIA NGAZI

    ReplyDelete
  55. Asante sana bwana Michuzi kwa kuipa hii article nafasi ya kupata mjadala mzuri. I just hope hata Raisi anasoma hii blog ya jamii. Vinginevyo tafadhali hakikisha anaona mjadala na maoni ya wadau wa blog ya jamii. Keep up the good work Mr Michuzi.

    ReplyDelete
  56. huyu anaongea kama vile yeye ndio mkuu wa nchi, huyu alipaswa afukuzwe kazi hata kabla hajamaliza hako ka press conference kake

    ReplyDelete
  57. Mdau hapo juu umesema kweli. JE TUTAJINASUAJE HAPA TULIPOFIKA. SISI WOTE WEZI, NI NANI WA KUMNYOOSHEA MWINGINE KIDOLE??? Hata viongozi wakuu wa umma ni wezi!!! Baba wa taifa Nyerere yote aliyofanya ni sifuri, tumekwenda kinyume na yote aliyofanya!!! Mimi nafikiri sasa hivi Tunahitaji kiongozi mwanamapinduzi (Revolutionary). Kiongozi kama Mao Zedong wa China, au Lenning wa USSR, ama Napoleon wa France. Otherwise we are dead as a country.

    ReplyDelete
  58. Sisi maprofessor ni watu tuna akili nzuri, ndio naana tumefikia ngazi ya kuwa professor. Ukiwa unaishi kama professor hapa Tanzania hata mtoto wako hutaweza kumsomesha shule ya private. Sasa kwa sababu tuna akili nzuri, tumeshagundua kwamba pesa iko kwenye siasa. Kwa hiyo kila mmoja wetu tunakimbilia kwenye siasa. Sio kwa sababu ya kuhudumia wananchi, bali ni kutafuta pesa. Sasa ninyi mnategemea nini? Haya masakata yote ya wizi ni mission zimepigiwa mahesabu ya kiprofessor. Ukiona sakata ambalo mistake imetokea mambo yakafahamika hiyo tunaita mathematicl error, ama grammatical error. Tutarekebisha hizi mistakes, na mwishowe hakuna kitunkitagundulika.

    ReplyDelete
  59. It is time to take responsibility.

    ReplyDelete
  60. Kwani kuwa waziri ndio kuwa juu ya sheria? Kama umetuhumiwa kwa kashfa achia ngazi ruhusu vyombo vya sheria vifanye kazi yake.

    ReplyDelete
  61. The wise people say" truth is such an awkward guest"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...