Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando (kushoto) akitoa neno la shukurani baada ya kusainiwa Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero na katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile.
Katibu Mkuu Wizara
ya fedha Bw. Servacius Likwalile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam wakati wa kusaini Mkataba wa mkopo
wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya
kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha
Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
(Picha zote na Eleuteri
Mangi – MAELEZO).
Na Eleuteri Mangi-
MAELEZO
12/12/2014.
Serikali ya Tanzania
imetiliana saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya Dola za
Kimarekani milioni 9.4 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 15.5 kutoka Benki ya
Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa
ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS).
Mkataba huo wa
makubaliano umesainiwa leo jijini Dara es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Muwakilishi wa
Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald
Kaberuka.
Dkt. Likwelile alisema kuwa
kituo hicho kitasaidia kupunguza tatizo la wataalam wa afya nchini na nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na hivyo kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi.
Kwa upande wake Muwakilishi
wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero ameipongeza Tanzania kuwa nchi ya kwanza
kusaini mkataba huo kati ya nchi nne za jumuiya ya EAC zinazokusudiwa kujenga
kituo kama hicho.
Bi Tonia alisema kuwa benki
ya ADB imejiwekea lengo kuboresha rasilimali watu katika fani ya afya ambapo
mradi wa ujenzi wa kituo kinachojengwa MUHAS upo katika mkakati wa benki hiyo
ambao uulianza 2011 hadi 2015, mpango mkakati wa benki wa 2013 hadi 2017 na
mfumo mpya wa elimu katka nchi za Afrika.
Mfumo huo unalenga kutatua
tatizo la utaalaam katika soko la ajira kwa kupitia vituo bora vya kanda vya
afya ili kuendana na dira ya maendeleo ya Taifa na mkakati wa kupunguza
umasikini ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mbando ameushukuru uongozi wa
benki ya ADB kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuahidi fedha hizo
zitatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Hadi kukamilika kwa
kituo hicho cha afya kinachojengwa katika chuo cha MUHAS kitagharimiwa na benki
ya ADB kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...