Na Bashir Yakub
Katika adhima ya ya mwendelezo wa makala za namna ya kuendesha
kampuni leo tena tuangalie kuhusu hisa
na hasa namna ya kuhamisha hisa.
HISA
NININI.
Kwa maana ambayo inaweza kueleweka kwa
wepesi zaidi ni kusema kuwa hisa ni aina ya maslahi ya mtu ya katika kampuni.Natumia
neno aina kwakuwa maslahi katika kampuni ni mengi si hisa tu isipokuwa hisa ni
mojawapo ya maslahi. Hivyo kile ambacho mtu anamiliki katika kampuni ndio hisa zake. Hisa hutofautiana kutokana na
uwezo wa mtu kwa maana wapo wenye hisa ndogo wapo wenye kubwa na kati.
KUUZA NA
KUNUNUA HISA.
Hisa ni mali inayohamishika. Ni mali sawa na mali nyingine zozote zinazohamishika.
Kama ambavyo mali
nyingine zinaweza kununuliwa au kuuzwa, kutolewa zawadi na kurithiwa ndivyo pia
hata hisa zinavyoweza kuwa.Hii yote huitwa kuhama kwa hisa. Kuhama kwa hisa kwa
lugha ya kitaalam ambayo ndio hutumika
katika katiba za makampuni ni ( Transfer of shares).
Mara nyingi suala la kuuziana hisa linawahusu wanahisa wenyewe na
hivyo wanahisa wanapokuwa wameuziana
hisa au wamepeana zawadi ni lazima
nyaraka inayoonesha muamala huo wa mauziano au zawadi ambayo ina muhuli wa
wakili iwasilishwe kwenye uongozi wa
kampuni kwa ajili ya kusajiliwa. Kama hakuna nyaraka yoyote iliyowasilishwa mbele ya
kampuni kuthibitisha uhamisho ni kosa kampuni kusajili uhamisho au mauziano
hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...