Bw. Lopez akiwasilisha hotuba jijini Addis Ababa

Na Ally Kondo, Addis Ababa


Uchumi wa Bara la Afrika umeelezwa kuwa unakua kwa kasi zaidi ukilinganisha na mabara mengine duniani. Hayo yamesemwa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Afrika, Bw. Carlos Lopez wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa AU jijini Addis Ababa, Ethiopia siku ya Jumatatu tarehe 26 Januari 2015.


Bw. Lopez alithibitisha kauli yake hiyo kwa kunakili ripoti mbalimbaliikiwa ni pamoja na ripoti ya Ernst & Young inayosema kuwa Bara la Afrika ni la pili kwa kuvutia uwekezaji baada ya Asia ya Kusini-Mashariki.

Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa uwekezaji baina ya nchi za Afrika umeongezeka na kwa sasa unakua kwa asilimia 32.4 kwa mwaka. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, jumla ya akiba ya fedha katika Bara la Afrika itafikia Dola za Marekani trilioni 23 kutoka trioni 12 ifikapo mwaka 2030.

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...