Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mbozi Bw. Elisey Ngowi akifungu semina ya
Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyoandaliwa na Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni katika Wilaya ya Mbozi Mkoa wa
Mbeya. Kushoto ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi
Ester Riwa na kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
Vijana wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya wakisikiliza kwa makini mafunzo yaliyokua
yakitolewa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo
ya Vijana iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni
katika Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa
kulia akifafanua jambo walipotembelea mradi wa kikundi cha vijana cha Miranaco wanaomiliki
duka la madawa muhimu katika Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya. Kushoto ni Afisa
Utamaduni Wilaya ya Mbozi Bw. Godfrey Msokwa, wapili kushoto ni Mkuu wa Kituo cha
Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na wapili kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha
Miranaco Bw. John Maige.
(Picha zote na Genofeva Matemu – Maelezo)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...