Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameituma
Saudi Arabia salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha
Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud (90) ambaye alifariki jana, Alhamisi, Januari 22, 2015, na kuzikwa leo, Ijumaa, Januari 23, 2015 mjini Riyadh.
Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud (90) ambaye alifariki jana, Alhamisi, Januari 22, 2015, na kuzikwa leo, Ijumaa, Januari 23, 2015 mjini Riyadh.
Katika
salamu zake kwa Mfalme mpya, Mfalme Salman bin Abdul Aziz al Saud, Rais Kikwete
amesema kuwa anaungana na wananchi wa Saudi Arabia na dunia nzima kuomboleza
kifo cha kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Saudi Arabia na
katika siasa za eneo la Mashariki ya Kati kwa jumla na kwa muda mrefu.
Ameongeza
Rais Kikwete: “Katika miaka yote 10 ya utawala wake tokea 2005 na kabla ya hapo
katika miaka mingine 10 wakati anashikilia utawala badala ya kaka yake Mfalme
Fahd aliyekuwa anaumwa, Mfalme Abdullah alithibitisha uongozi wa kuwajibika na
msimamo thabiti wa kutafuta amani katika Mashariki ya Kati na dunia itaendelea
kumkumbuka kwa mchango huo.”
Amesisitiza
Mhe. Rais Kikwete: “Aidha, sisi katika Tanzania
tutaendelea kuenzi juhudi zake kubwa za kujenga na kuimarisha uhusiano wa karibu
kati ya nchi zetu,” amesema Rais Kikwete.
“Kwa
niaba ya wananchi wa Tanzania, Serikali ninayoiongoza na mimi mwenyewe,
nakutumia wewe Mfalme Salman salamu za rambirambi, na kupitia kwako kwa
wananchi wote wa Saudi Arabia kwa kuondokewa na kiongozi wao. Sisi katika Tanzania tunaungana nanyi
kuomboleza na kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya
Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud. Amen.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
23 Januari,2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...