Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana ukikatiza mapema jioni ya leo katikati ya msitu ukielekea katika
kijiji cha Mnarani -Makangale kuzungumza na wanachama wa chama
hicho,micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya Vijana wapatao 105
waliokuwa chama cha CUF na kuhamia CCM,katika kijiji cha Mnarani
Makangale,ambapo alikwenda kushiriki ujenzi wa tawi lao liitwalo Maskani
tuheshimiane.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Vijana wapatao 105 waliokuwa
chama cha CUF na kuhamia CCM.Wakisoma taarifa yao kwa Ndugu Kinana
walieleza manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CUF,walieleza
kuwa tangu wamehama chama hicho wamekuwa wakibugudhiwa na kufanyiwa
fujo kiasi ambacho wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao za kimaendeleo
ikiwemo na shughuli zao za uvuvi kusimama,hivyo wamemuomba Katibu Mkuu
wa CCM,Ndugu Kinana kulishughulikia jambo hilo ili waweze kuendelea na
shughuli zao bila kubugudhiwa kwani wanataka kuishi kwa amani na
utulivu.
Akizungumza Ndugu Kinana alisema kuwa chama cha CUF
hakitendi haki katika suala zima la demokrasia, ''kwani kila mtu ana
uhuru wa kuhamia chama anachotaka na haitaji kubugudhiwa,hivyo Viongozi
wa CUF,wanapaswa kulitambua hilo na kuwaacha wananchi waamue watakavyo
ili mradi hawavunji sheria za nchi wala kumbugudhi mtu'' alisema Kinana.
Kinana
yupo katika ziara ya siku tano ya Kikazi kisiwani Pemba,akihimiza na
kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni
pamoja na kukagua uhai wa chama kisiwani humo.
Baadhi
akina mama Wakulima wa Mpunga wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana aliyekwenda Bonde la Mpunga Koowe kuangalia na
kushiriki ujenzi wa tuta la Kuzuia maji chumvi katika bonde hilo.
Pichani
kati ni Afisa Mkuu wa Idara ya Umwagiliaji maji-Pemba Mbarouk Ali Mgau
akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda bonde la Mpunga Koowe-wingwi, kuangalia na kushiriki ujenzi wa tuta la Kuzuia maji chumvi katika bonde hilo.Afisa Mbarouk alieleza kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 170 zilizotolewa na TASAF.
Ndugu
Kinana akiwa na baadhi ya akina Mama ambao ni wakulima wa zao la Mpunga
katika Bonde la Koowe,wakishiriki ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi
katika bonde hilo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya Madaktari wa hospitali ya Wilaya ya
Micheweni,mara baada ya kuwasili katika hospitali hiyo,Kaskazini Pemba mapema leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akipata maelezo kutoka kwa Dkt.Rashid Daud Mkasha Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Micheweni wakati alipokuwa akikagua ukarabati wa wodi katika
hospitali hiyo. Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya,Dkt.Rashid alieleza kuwa hospitali hiyo ilikuwa ya kijiji na sasa imepandishwa hadhi kuwa hospitali ya Wilaya,hivyo mradi wa ujenzi wa wodi ya Wanaume na Akina Mama unaendelea kwa kasi ili kuendana na vigezo.
PICHA NA MICHUZI JR-MICHEWENI-KASKAZINI PEMBA
Huku viongozi wa ccm wakiendelea na ziara za kuvuna wanachama, eti baadhi ya viongozi wa Ukawa wanafanya maandamano na kukamatwa. Tumieni akili wanayotumia ccm. Mambo ya kukamatwa na kupelekwa police niny watu wazima na viongozi ni aibu sana. Police si mahali pazuri na kama kiongozi hupaswi kuwa na record kwamba ulikamatwa na kuwekwa lumande. Tendeni haki kwa watu, vurugu hazifai katika jamii.
ReplyDeleteDemocracy,people should be allowed to demonstrate as long as they are not breaking any law,if you deny demonstration means you deprive a constitutional right of a citizen
ReplyDelete