Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana sambamba na Wananchi wakishiriki ujenzi wa Madarasa ya Skuli ya Uwandani,katika jimbo la Wawi,wilaya ya Chake Chake,Mkoa Kusini Pemba.Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa mbele ya katibu Mkuu Ndugu Kinana,imeeleza kuwa mradi wa ujenzi wa jengo hilo litakalokuwa na jumla ya vyumba sita,litagharimu kiasi cha shilingi milioni 18 zitakazomilisha mradi huo.
 Katibu Mkuu wa CCM na ujumbe wake pamoja na wananchi wakikatiza kwenye shamba la miti linalosimamiwa na Kikundi cha Utunzaji Mazingira kiitwacho Hatugombani Cooperative,kilichopo Kilindi,Wilaya ya Chake Chake,mkoa wa Kusini Pemba.Kikundi hicho kina jumla ya Wanachama wapatao 49,ambapo shughuli kubwa ya kikudi hicho ni utunzaji wa mazingira kwa upandaji miti ya Mivinje,Mikaratusi,Mikungu na Mitondoo.Mradi huo wa kuhifadhi Mazingira una eneo la eka 20,ambapo mpaka sasa mradi huo una thamani ya shilingi Milioni 40 na zaidi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akishiriki kupanda mti katika shamba la miti linalosimamiwa na Kikundi cha Utunzaji Mazingira kiitwacho Hatugombani Cooperative,kilichopo Kilindi,Wilaya ya Chake Chake,mkoa wa Kusini Pemba.Kikundi hicho kina jumla ya Wanachama wapatao 49,ambapo shughuli kubwa ya kikudi hicho ni utunzaji wa mazingira kwa upandaji miti ya Mivinje,Mikaratusi,Mikungu na Mitondoo.Mradi huo wa kuhifadhi Mazingira una eneo la eka 20,ambapo mpaka sasa mradi huo una thamani ya shilingi Milioni 40 na zaidi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kuotesha miche ya Mikarafuu katika bustani ya kikunndi cha Hatukosani,wakati alipotembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na kikundi hicho chenye wanachama wapatao 25 kilichopo Chanjamjawiri-Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipewa taarifa ya kikundi cha Ushirika cha Jitihada Mbele cha Ufugaji  wa Samaki chenye jumla ya wanachama 10.Kikundi hicho kilianzishwa kwa lengo la Ufugaji wa samaki ili waweze kujikwamua kiuchumi na pia kusimamia sera ya chama cha CCM,ikiwemo kujikusanya kwa pamoja ili kuanzisha vikundi vya ushirika kwa ajili ya kujiajiri wenyewe.Kwa Mujibu wa Msomaji wa taarifa alieleza kuwa mradi huo wa samaki una jumla ya thamani ya shilingi milioni 10.
 Mfuasi wa Chama cha CUF Ghalib Bedui Khamis akikabidhi kadi yake kwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya uanachama wa CCM.
 Mfuasi wa Chama cha CUF Said Abdallah Ibrahim akionesha kadi yake ya zamani kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kabla ya kukabidhi na kupewa kadi mpya ya uanachama wa CCM,mbele ya Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Pujini Kunvini Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba. 

PICHA NA MICHUZI JR-CHAKE CHAKE-KUSINI PEMBA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...