Watu wenye uhitaji wa msaada wa sheria sasa wanaweza kupata huduma hiyo kwa
kuingia mtandaoni baada ya wakili mmoja Jijini Dar es Salaam kuanza kutoa huduma
hiyo.
Wakili Emmanuel Augustino ameanza kuwafikia wahitaji wa msaada wa sheria kwa
kutumia blog yake ya wakiliwangu.blogspot.com.
"Kupitia blog hii, tunatoa ushauri wa kisheria wa mambo yanayohusu mirathi, ununuzi au
uuzaji wa ardhi, kesi za jinai na madai, kuanzisha kampuni na mambo mengine tofauti ya
kisheria," alisema Wakili Augustino.
Wakili Augustino anasema kuwa wazo la kutoa msaada wa kisheria kwa njia ya mtandao
lilimjia baada ya kuhudhuria mkutano mkuu wa chama cha wanasheria wa Afrika
Mashariki kilichofanyika Kigali, Rwanda mwaka huu.
"Kule Kigali, kulikuwa na mjadala kuhusu matumizi ya teknologia kuwafikia wateja.
Wanasheria maarufu walisema kuwa ni namna bora ya kuwafikia watu, badala ya
utaratibu tuliouzowea wa kufuatwa ofisini," alisema.
"blog ya wakiliwangu.blogspot.com ni kwa ajili ya watu wasio na uwezo. Tunachokifanya
ni kutoa ushauri na pia msaada wa kuandika nyalaka tofauti zinazohitajika kukamilisha
mchakato wa kisheria kama kuandika wosia, kuandika mikataba, n.k. Tunatoa msaada
kwa njia ya simu, email," aliongeza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...