Picha na habari na Faustine Rutta
Ligi Kuu ya Vodacom imeendelea Jumamosi  kwa Mechi kadhaa na Mabingwa Watetezi Azam FC kushinda huko Shinyanga na kutwaa uongozi wa Ligi toka kwa Mtibwa Sugar ambao wanacheza leo, huku Yanga wakiteleza kutwaa uongozi huo baada ya kubanwa na Ruvu Shooting kwa Sare ya 0-0 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga walistahili ushindi lakini walishindwa kufunga wakati walipata nafasi za wazi kibao.

Huko Kambarage, Shinyanga, Azam FC wameifunga Stand United Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 43 la Frank Domayo na kukaa kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 1 mbele ya Mtibwa Sugar ambao wanacheza Jumapili Ugenini na JKT Ruvu.

Huko CCM Kirumba, Mwanza, Mbeya City wameifunga Kagera Sugar, wanaotumia Uwanja huo kwa Mechi za Nyumbani baada Kaitaba kufungwa kwa ukarabati, Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 84 la Peter Mapunda.

Nao Simba wameichapa Ndanda FC waliokuwa kwao Uwanja Nangwanda Bao 2-0 kwa Bao za Dan Sserunkuma na Elias Maguri.
Mchezaji wa Mbeya City akiondosha mpira kenye eneo la hatari walipokipiga na Kagera Sugar Uwanja wa CCM kirumba na kushinda bao 1-0.
Mashabiki wa Mbeya City wakishangilia bao baada ya Timu yao kupata bao katika dakika za Mwishoni dakika ya 84 dhidi ya Kagera Sugar.
Langoni mwa Timu ya Mbeya City wakiusubiri mpira wa kona.
Kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi akihojiwa na Baadhi ya Waandishi wa Habari kwenye Uwanja wa Kaitaba jioni ya leo baada ya Timu yake kuibuka na Ushindi wa bao 1-0 Dhidi ya Kagera Suagar ya mjini Bukoba. Picha na Faustine Ruta wa Bukobasports.com
Raha ya Ushindi wa Mbeya City jijini Mwanza jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...