Meneja Tawala wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Gabriel Madembwe (katikati) akiwahutubia Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi yaliyofanyika leo mkoani Morogoro. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Frank Mkumbo na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Bw. Edward Kaluvya.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua habari wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Frank Mkumbo akiwa katika mahojiano na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...