Mwenyekiti wa Chuo cha Karate nchini Tanzania,Willy Ringo ameyataka mashirika na makampuni nchini kuunga mkono mchezo wa Karate ili kufika mbali zaidi ulimweguni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam,Rwezaula ameitaka Serikali pamoja na Makampuni yeyote  kuusaidia mchezo huo wa Karate,pia ameitaka Serikali kuacha kudhamini michezo mingine kama mpira wa miguu na mashindano ya urembo.

Kwa upande wake, Bingwa wa Dunia katika mchezo wa Karate, Rutashobya Ringo amewataka Watanzania kuwa na nidhamu pamoja na kumuamini Mungu katika mchezo wowote ili kujihakikishia ushindi.
 Mwenyekiti Chuo cha Karate Tanzania Willy Ringo Rwezaula akionesha mmoja cheti alichokipata baada ya kushinda moja ya mashindano nje ya nchi ndugu Rutashobya Ringo.
 Rutashobya Ringo akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuonesha vyeti vyake pamoja na kombebaada ya kushinda nchini Urusi. Pia ameeleza kuwa anakwenda kushiriki olympic nchini Brazil kwenye mshindano ya Karate.
 Bwana Dormidontov Vadim ambaye ni mwalimu wa mchezo wa Karate nchini Urusi akizungumza jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...